12 – Muhammad bin Kathiyr ametuhadithia: Sufyaan ametukhabarisha, kutoka kwa Habiyb, kutoka kwa Abul-´Abbaas, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhumaa), ambaye amesema:

”Bwana mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema: ”Nikapambane jihaad?” Akasema: ”Wazazi wako wanaishi?” Akasema: ”Ndio.” Ndipo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Basi kapambane kwao.”

13 – Abu Nu´aym ametuhadithia: Sufyaan ametukhabarisha, kutoka kwa ´Atwaa’ bin as-Saa-ib, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr, ambaye amesema:

”Bwana mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumpa kiapo cha usikivu juu kuhajiri, na huku nyuma amewaacha wazazi wawili wakilia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: ”Rudi kwao na uwachekeshe kama ulivyowaliza.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 112
  • Imechapishwa: 16/12/2024