2 – Kila mmoja katika wao akataja kitu cha jumla kupitia baadhi ya sifa zake kwa namna ya kutolea mfano na kuzindua na si kwa namna ya kutoa maelezo kamili yanayolingana na jina hilo kwa ujumla wake au mahsusi. Kwa mfano mgeni ambaye haelewi maana ya neno mkate akaonyeshwa mkate bapa. Hii ni ishara ya aina fulani ya mkate, si mkate huo peke yake. Mfano wa hilo ni maneno Yake (Ta´ala):
ثُمَّ أَوْرَثْنَا الْكِتَابَ الَّذِينَ اصْطَفَيْنَا مِنْ عِبَادِنَا ۖ فَمِنْهُمْ ظَالِمٌ لِّنَفْسِهِ وَمِنْهُم مُّقْتَصِدٌ وَمِنْهُمْ سَابِقٌ بِالْخَيْرَاتِ بِإِذْنِ اللَّـهِ
“Kisha Tukawarithisha Kitabu wale tuliowateuwa miongoni mwa waja Wetu. Basi miongoni mwao ni aliyedhulumu nafsi yake na miongoni mwao aliyekuwa kati na kati na miongoni mwao aliyetangulia kwa mambo ya kheri kwa idhini ya Allaah.”[1]
Inafahamika kwamba anayejidhulumu nafsi yake anapuuza mambo ya wajibu na anayafanya mambo ya haramu, aliye kati na kati anafanya mambo ya wajibu na kuepuka mambo ya haramu na aliyetangulia anafanya yale yanayopendeza na yale mambo ya wajibu. Wale watu wa kati na kati ni wale watu wa upande wa kulia:
وَالسَّابِقُونَ السَّابِقُونَ أُولَـٰئِكَ الْمُقَرَّبُونَ
“Waliotangulia mbele – watatangulia mbele. Hao ndio watakaokurubishwa.”[2]
Baada ya hapo kila mmoja katika wao akafasiri aliyetangulia kwa aina fulani ya utiifu. Mmoja akasema kuwa aliyetangulia ni yule mwenye kuswali mwanzoni mwa wakati, wa kati na kati ni yule anayeswali katikati ya wakati wa swalah na aliyeidhulumu nafsi yake ni yule anayechelewesha ´Aswr mpaka pale jua linapokua manjano. Mwingine akasema kuwa aliyetangulia na wa kati na kati wametajwa mwanzoni mwa Suurah ya al-Baqarah ambapo mtenda wema amefungamanishwa na swadaqah, mwenye kuidhulumu nafsi yake amefungamanishwa na ribaa na mwenye kujifanyia uadilifu amefungamanishwa na kufanya biashara. Watu inapokuja katika suala la mali wamegawanywa katika makundi matatu: wafanya ihsani, waadilifu au madhalimu. Mtu aliyetangulia ni yule mwenye kufanya ihsani kwa kutekeleza yale mambo yanayopendeza pamoja na yale mambo ya wajibu, aliyeidhulumu nafsi yake ni mwenye kula ribaa au anayezuia zakaah, aliye kati na kati ni yule anayetoa swadaqah iliyofaradhishwa na hali ribaa. Inahusiana na mifano ya maono haya. Kila moja katika maoni yametaja sifa inayoingia ndani ya Aayah. Imetajwa kwa namna ya kielelezo na ufahamishaji, kwa sababu inakuwa rahisi kwa msikilizaji kuelewa mfano kuliko utambulisho wa kulengesha. Akili timamu inaelewa aina kama inavyoelewa kipi kinachokusudiwa wakati kunapoulizwa kuhusu mkate na kukaashiriwa mkate bapa.
[1] 35:32-33
[2] 56:10-11
- Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 31-34
- Imechapishwa: 21/03/2025

Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 31-34
Imechapishwa: 21/03/2025
https://firqatunnajia.com/04-tafsiri-ya-qur-aan-kupitia-mifano/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket