34 – Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
“Hakika ndani ya usiku kuna saa ambayo hakuna mtu muislamu anayoafikiana nayo ambaye anamuomba Allaah (Ta´ala) kheri yoyote katika mambo ya kidunia na Aakhirah, isipokuwa Allaah humpa. Hilo linakuwa katika kila usiku.”[1]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Hadiyth inafahamisha kuwa miongoni mwa fadhilah na wema wa Allaah ni kwamba ametufanyia saa ya kuitikiwa ambayo hakuna mja yeyote anayemuomba Allaah isipokuwa humuitikia. Hapo ni pale ambapo yanatimia masharti ya kuitikiwa du´aa. Kwa msemo mwingine ni kwamba asiombe kwa jambo lenye dhambi au kukata udugu.
Allaah (Ta´ala) ametuficha saa hiyo ili mja ajitahidi katika kila usiku. Ni kama ambavo Allaah ameificha saa ilioko siku ya ijumaa ili waja waweze kujitahidi mchana wake wote.
[1] Muslim (757).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 38
- Imechapishwa: 08/10/2025
34 – Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
“Hakika ndani ya usiku kuna saa ambayo hakuna mtu muislamu anayoafikiana nayo ambaye anamuomba Allaah (Ta´ala) kheri yoyote katika mambo ya kidunia na Aakhirah, isipokuwa Allaah humpa. Hilo linakuwa katika kila usiku.”[1]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Hadiyth inafahamisha kuwa miongoni mwa fadhilah na wema wa Allaah ni kwamba ametufanyia saa ya kuitikiwa ambayo hakuna mja yeyote anayemuomba Allaah isipokuwa humuitikia. Hapo ni pale ambapo yanatimia masharti ya kuitikiwa du´aa. Kwa msemo mwingine ni kwamba asiombe kwa jambo lenye dhambi au kukata udugu.
Allaah (Ta´ala) ametuficha saa hiyo ili mja ajitahidi katika kila usiku. Ni kama ambavo Allaah ameificha saa ilioko siku ya ijumaa ili waja waweze kujitahidi mchana wake wote.
[1] Muslim (757).
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 38
Imechapishwa: 08/10/2025
https://firqatunnajia.com/04-saa-ambayo-mtu-anaitakiwa-maombi-yake-usiku/