7 – Imaam Abu Sulaymaan Daawuud bin ´Aliy ametusimulia:

”Tulikuwa kwa Ibn-ul-A´raabiy wakati alipokuja bwana mmoja na akasema: ”Nini maana ya maneno ya Allaah (Ta´ala):

الرَّحْمَنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَى

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi?”[1]

Akajibu: ”Yuko juu ya ´Arshi kama alivyoeleza.” Akasema: ”Ee Abu ´Abdillaah! Sio maana yake. Maana yake ni kwamba ametawala (استولى).” Akasema: ”Nyamaza. Hakuna ambaye anakitawala kitu isipokuwa ni lazima awe na mpinzani. Anaposhinda mmoja wao ndio husemwa kuwa ametawala.”[2]

8 – Ibn Wahb amesema:

”Tulikuwa kwa Maalik ambapo akaingia bwana mmoja na kusema:

الرَّحْمَنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَى

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi”

Amelingana vipi?” Maalik akainamisha kichwa chake kitambo kirefu na akaanza kutokwa na jasho. Kisha akasema: ”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi, kama alivyojielezea Mwenyewe. Kwa hivyo haitakiwi kuuliza vipi, kwa sababu haina maana kwa nisba Yake. Wewe ni mzushi. Mtoeni nje!”

9 – Hayo yamesemwa pia na Rabiy´ah, mwalimu wake Maalik, na yamepokelewa kutoka kwa Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) na Ibn Wahb.

10 – ´Aliy bin al-Hasan bin Shaqiyq amesema:

”Nilimuuliza ´Abdullaah bin al-Mubaarak: ”Tutamjua vipi Mola wenu?” Akasema: ”Kwamba Yuko juu ya mbingu ya saba, juu ya ´Arshi Yake. Haitakiwi kusema kama wanavosema Jahmiyyah, kwamba Yuko hapa ardhini.”

Wakati alipoambiwa haya Ahmad bin Hanbal, akajibu:

”Nasi pia tunasema hivo.”[3]

11 – ´Abdur-Rahmaan bin Mahdiy amesema:

”Jahmiyyah wanachotaka ni kupinga kuwa Allaah amemzumgumzisha Muusa na kwamba Mwingi wa huruma amelingana juu ya ´Arshi. Naona kuwa wanatakiwa kutubu. Ima watubu na vinginevyo wakatwe mashingo yao.”[4]

12 – al-Aswma´iy amesema:

“Mke wa Jahm alifika wakati bwana mmoja alipomwambia kuwa Allaah yuko juu ya ´Arshi. Ndipo akasema: “Aliyefupika juu ya kilichofupika?” Mwanamke huyu amekufuru kutokana na matamshi haya.”

13 – al-Awzaa´iy amesema:

“Tulikuwa, wakati ambapo wanafunzi wa Maswahabah wamejaa, tukisema: “Allaah (Ta´ala) yuko juu ya ´Arshi Yake na tukiamini zile sifa Zake zilizotajwa katika Sunnah.”[5]

14 – Sa´iyd bin ´Aamir adh-Dhwab´iy – imamu wa Baswrah – amesema:

”Watu wa dini zote na waislamu wameafikiana juu ya kwamba Allaah yuko juu ya ´Arshi. Lakini Jahmiyyah wanasema: ”Juu ya ´Arshi hakuna chochote.”

15 – ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) amesema katika ´Aqiydah na wasia wake:

”Ile ´Aqiydah ambayo ninafuata na nimewaona maswahiba zetu, Ahl-ul-Hadiyth kama vile Sufyaan na Maalik, wakiifuata na ambayo naikubali, inahusiana na kukiri ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah… na kwamba Allaah yuko juu ya ´Arshi Yake juu ya mbingu Yake. Anawakaribia viumbe Wake vile anavyotaka na anashuka katika mbingu ya chini vile anavotaka… ”

16 – Bishr al-Haafiy amesema:

”Tunaamini kuwa Allaah amelingana juu ya ´Arshi kama Anavyotaka na kwamba anao utambuzi wa kila mahali.”

17 – ´Uthmaan bin Sa´iyd ad-Daarimiy amesema:

”Waislamu wameafikiana ya kwamba Allaah yuko juu ya ´Arshi Yake na juu ya mbingu Zake.”

18 – Kusema kwamba Allaah (Ta´ala) yuko juu ya ´Arshi ni jambo limesimuliwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia kwa Jubayr bin Mutw´im, al-´Abbaas bin ´Abdil-Muttwalib, Abu Hurayrah, Sa´d bin Abiy Waqqaas, Jaabir bin ´Abdillaah, Anas bin Maalik, Ibn ´Abbaas, Qataadah bin an-Nu´maan, ´Ubaadah bin as-Swaamit, Ibn Mas´uud na Jaabir bin Sulaym. Hayo pia yamesimuliwa kutoka kwa Maswahabah wengi na wanafunzi wao.

Katika vile vitabu vya kale miongoni mwa yaliyomo ni kama yale yaliyosihi kwamba Ka´b al-Ahbaar anasema katika Tawraat:

”Mimi ni Allaah juu ya waja Wangu. Niko juu ya ´Arshi na nayaendesha mambo ya waja Wangu.”

[1] 20:5

[2] al-Albaaniy amesema:

”Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh kutoka kwake. Ibn Naftuuyah an-Nahawiy ameyatumia kama hoja katika ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”.” (Mukhtaswar-ul-´Uluww, uk. 31)

[3] Twabaqaat-ul-Hanaabilah (2/233).

[4] Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

”Miongoni mwa kuondosha yenye kuudhi ni kusafisha walinganiaji wa upotofu. Hata hivyo hiyo sio kazi yetu; mamlaka ndio wenye kufanya hivo.” (Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 266)

[5] al-Asmaa’ was-Swifaat (2/150).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy (afk. 748)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 38-45
  • Imechapishwa: 28/05/2024