6 – Abu ´Abdillaah Muhammad bin ´Abdil-Waahid bin Ahmad at-Twarqiy ametukhabarisha huko Karkh: Abu Bakr ´Umar bin Ibraahiym bin Marduuyah al-Karkhiy ametuhadithia: Abaan bin Ja´far bin Abiy Ja´far an-Najiyramiy ametuhadithia: Ahmad bin Sa´d ath-Thaqafiy al-Mutwawwi´iy ametuhadithia: Sufyaan bin ´Uyaynah ametuhadithia: Ibraahiym bin Maysarah ametukhabarisha, kutoka kwa Anas, aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Jifunzeni elimu, muifanyie kazi kwa vitendo na muifunze. Msiwape watu wasioiistahiki na msiwanyime wale wenye kuiistahiki.”[1]

7 – Abul-Hasan Muhammad bin Ahmad bin Muhammad bin Ahmad bin Rizq al-Bazzaar ametukhabarisha: Abu ´Amr ´Uthmaan bin Ahmad bin ´Abdillaah ad-Daqqaaq ametuhadithia: ´Abdullaah bin Muhammad bin Ismaa´iyl bin at-Tabbaan al-Baswriy ametuhadithia: Muhammad bin Abiy Bakr al-Muqaddamiy ametuhadithia: Bishr bin ´Abbaad ametuhadithia, kutoka kwa Bakr bin Khunays: Hamzah an-Naswiybiy amenihadithia, kutoka kwa Yaziyd bin Yaziyd bin Jaabir, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Mu´aadh bin Jabal, aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Jifunzeni yale mnayotaka kuyajua. Allaah (Ta´ala) hatokunufaisheni mpaka myafanyie kazi kwa vitendo yale mliyojifunza.”[2]

8 – Muhammad bin Abiy ´Aliy al-Aswbahaaniy amenikhabarisha: Haafidhw Ahmad bin Hamdaan ash-Shiyraaziy ametukhabarisha: Muhammad bin Muhammad bin Sulaymaan al-Baaghandiy ametuhadithia: ´Aliy bin al-Madiyniy ametuhadithia: ´Uthmaan bin ´Abdir-Rahmaan al-Jumahiy ametuhadithia, kutoka kwa Yaziyd bin Yaziyd bin Jaabir, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Mu´aadh bin Jabal, aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Jifunzeni yale mnayotaka kuyajua. Allaah hatokulipeni ujira mpaka myafanye matendo.”[3]

[1] Mwongo kwa sababu ya huyu Abaan bin Ja´far. adh-Dhahabiy amesema:

”Mwongo. Alikuwa akiishi Baswrah.” (Dhayl-udh-Dhwu´afaa’)

Hakumtaja katika ”Miyzaan-ul-I´tidaal”, ndiyo maana Haafidhw Ibn Hajar akamdiriki katika “Lisaan-ul-Miyzaan” na akasema kwamba jina Abaan ni matokeo ya kosa la chapa na kwamba sahihi ni kwamba anaitwa Abaa´. Kwa jina hilo ndivo adh-Dhahabiy amemtaja katika “Miyzaan-ul-I’tidaal”.

Inasemekana kuwa Ibn Hibbaan amesema kuwa bwana huyo amemzulia Imaam Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah) zaidi ya Hadiyth 300. Haafidhw Ibn Hajar amezidisha katika ”Lisaan-ul-Miyzaan”:

”Hamzah amesimulia kuwa al-Hasan bin ´Aliy bin Ghulaam az-Zuhriy amesema: ”Abaa´ bin Ja´far alikuwa akitunga Hadiyth. Katika nakala yake moja amesimulia karibu Hadiyth mia moja kutoka kwa mwalimu wake asiyejulikana, ambaye alikuwa akimwita Ahmad bin Sa´d bin ´Amr al-Mutwawwi´iy, kutoka kwa Ibn ´Uyaynah, kutoka kwa Ibn Maysarah, kutoka kwa Anas. Humo mna Hadiyth za munkari na zisizotambulika. Abul-Haarith amesimulia sana kutoka kwake katika ”al-Musnad” ya Abu Haniyfah.

[2] Cheni yake ya wapokezi ni dhaifu sana. Hamzah bin Abiy Hamzah an-Naswiybiy alikuwa mwenye kuachwa na mwenye kutuhumiwa kutunga. Bakr bin Khunays alikuwa mwenye kuaminika lakini mwenye kukosea. Imekuja katika ”at-Taqriyb” ya kwamba Ibn Hibbaan alikuwa akichupa mipaka kwake. adh-Dhahabiy amemtaja katika ”Miyzaan-ul-I´tiqaad” na akasema:

”ad-Daaraqutwniy amesema: ”Ni mwenye kuachwa.”

[3] Dhaifu kwa sababu ya al-Jumaahiy. Ibn ´Adiy amesema juu yake:

”Mengi katika aliyosimulia ni dhaifu na munkari.”

ad-Daarimiy ameipokea katika “as-Sunan” yake (1/81) kupitia kwa Sa´iyd bin ´Abdil-´Aziyz, kutoka kwa Yaziyd bin Jaabir, kutoka kwa Mu´aadh. Ameipokea kwa njia ya maneno ya Mu´aadh, na hivo ndio sahihi.

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 19-21
  • Imechapishwa: 07/05/2024
  • Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy