Haya yaliyotajwa hapo juu hayasimami sawa kwa mja isipokuwa kwa kusimama sawa moyo wake na viungo vyake. Kusimama sawa kwa moyo kunakuwa kwa mambo mawili:
1 – Kupenda kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kuwe mbele kwa mja kuliko mapenzi yote mengine. Basi mapenzi ya Allaah yakigongana na mapenzi ya mwingine, basi mapenzi ya Allaah yawe ndiyo yanayotangulia moyoni mwake na aweke juu ya hilo matokeo yanayolingana nayo. Ni rahisi sana kusema hivi kwa madai, lakini ni jambo gumu sana kulitekeleza kwa vitendo. Kwa sababu wakati wa mtihani ndipo mtu huheshimiwa au hudhalilishwa. Ni mara nyingi sana mja kuweka mbele kile anachokipenda yeye au anachokipenda mkubwa wake, kiongozi wake, Shaykh wake au jamaa zake kuliko kile anachokipenda Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Huyu basi hajafanya mapenzi ya Allaah kuwa ya mbele moyoni mwake kuliko mapenzi yote wala haijawa mapenzi hayo ndio malkia inayoamrisha juu ya mapenzi mengine. Sunnah ya Allaah (´Azza wa Jall) kwa mwenye hali kama hii ni kwamba humharibia hayo anayoyapenda na humfanyia maisha ya mashaka kwayo na hampati chochote katika hayo isipokuwa kwa tabu na karaha, kuwa ni malipo kwa kutanguliza matamanio yake au matamanio ya yule anayemuheshimu miongoni mwa viumbe kuliko mapenzi ya Allaah. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amehukumu hukumu isiyoweza kurejeshwa wala kuzuilika kwamba anayependa kitu chochote kinyume na Yeye basi lazima ataadhibiwa nacho. Anayemwogopa mwingine kinyume na Yeye basi atatawaliwa naye. Anayejishughulisha na kingine badala Yake basi jambo hilo litakuwa ni la kumletea mkosi. Anayempa kipaumbele mwingine zaidi Yake basi hatabarikiwa katika jambo hilo. Anayemridhisha mwingine kwa kumchukiza Yeye basi Yeye atamchukia na hilo haliwezi kuepukwa.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 14
- Imechapishwa: 28/07/2025
Haya yaliyotajwa hapo juu hayasimami sawa kwa mja isipokuwa kwa kusimama sawa moyo wake na viungo vyake. Kusimama sawa kwa moyo kunakuwa kwa mambo mawili:
1 – Kupenda kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kuwe mbele kwa mja kuliko mapenzi yote mengine. Basi mapenzi ya Allaah yakigongana na mapenzi ya mwingine, basi mapenzi ya Allaah yawe ndiyo yanayotangulia moyoni mwake na aweke juu ya hilo matokeo yanayolingana nayo. Ni rahisi sana kusema hivi kwa madai, lakini ni jambo gumu sana kulitekeleza kwa vitendo. Kwa sababu wakati wa mtihani ndipo mtu huheshimiwa au hudhalilishwa. Ni mara nyingi sana mja kuweka mbele kile anachokipenda yeye au anachokipenda mkubwa wake, kiongozi wake, Shaykh wake au jamaa zake kuliko kile anachokipenda Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Huyu basi hajafanya mapenzi ya Allaah kuwa ya mbele moyoni mwake kuliko mapenzi yote wala haijawa mapenzi hayo ndio malkia inayoamrisha juu ya mapenzi mengine. Sunnah ya Allaah (´Azza wa Jall) kwa mwenye hali kama hii ni kwamba humharibia hayo anayoyapenda na humfanyia maisha ya mashaka kwayo na hampati chochote katika hayo isipokuwa kwa tabu na karaha, kuwa ni malipo kwa kutanguliza matamanio yake au matamanio ya yule anayemuheshimu miongoni mwa viumbe kuliko mapenzi ya Allaah. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amehukumu hukumu isiyoweza kurejeshwa wala kuzuilika kwamba anayependa kitu chochote kinyume na Yeye basi lazima ataadhibiwa nacho. Anayemwogopa mwingine kinyume na Yeye basi atatawaliwa naye. Anayejishughulisha na kingine badala Yake basi jambo hilo litakuwa ni la kumletea mkosi. Anayempa kipaumbele mwingine zaidi Yake basi hatabarikiwa katika jambo hilo. Anayemridhisha mwingine kwa kumchukiza Yeye basi Yeye atamchukia na hilo haliwezi kuepukwa.
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 14
Imechapishwa: 28/07/2025
https://firqatunnajia.com/04-mapenzi-ya-allaah-rahisi-kusema-vigumu-kuyaonyesha-kivitendo/