4- Du´aa wakati wa kutoka nyumbani
Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mtu akitoka kwenye nyumba yake akasema:
بِسْمِ اللهِ تَوَكَّلْتُ عَلى اللهِ وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ تَعَالى
“Kwa jina la Allaah. Nimemtegemea Allaah. Hapana namna wala nguvu isipokuwa kwa msaada Allaah (Ta´ala).”
basi hapo huambiwa: “Umeongozwa, umetoshelezwa na kulindwa.” Shaytwaan hujiepusha naye na kuwaambia mashaytwaan wengine: “Ni vipi mtamuweza mtu ambaye ameongozwa, kutoshelezwa na kulindwa?”[1]
[1] Abu Daawuud.
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Ashru Waswaayaa lil-Wiqaayah min-al-Wabaa’, uk. 8
- Imechapishwa: 30/03/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)