Yule mwenye kufuata mfumo wa Salaf anahitajia mambo mawili yafuatayo:
1 – Autambue mfumo wa Salaf.
2 – Kushikamana nao bila kujali shida utazopata. Mtu atapata maudhi, matusi, tuhuma na majina ya kebehi kutoka kwa wapinzani. Pamoja na hivyo mtu anatakiwa awe na subira juu ya hayo, kwa sababu yuko na uhakika wa kile alichomo. Asitikiswe na vimbunga na wala fitina zisimbadilishe. Aubiri juu ya hayo mpaka atapokutana na Mola Wake.
Mosi mtu anatakiwa kusoma mfumo wa Salaf. Pili awafuate kwa wema. Tatu awe na uvumilivu kwa yatayomkumba kutoka kwatu. Haya hayatoshelezi vilevile, ni lazima kueneza ´Aqiydah ya Salaf, ni lazima alinganie kwa Allaah, alinganie katika ´Aqiydah ya Salaf, awabainishie watu, ayaeneze kati ya watu. Huyu ndiye Salafiy wa kihakika. Mwenye kudai Salafiyyah naye hajui mfumo wa Salaf au akawa anatambua lakini akawa haufuati, bali yeye anafuata yale waliyomo watu, au anafuata yale yenye kuendana sambamba na matamanio yake huyu sio Salafiy. Haijalishi kitu hata kama atajiita “Salafiy”. Mtu wa sampuli nyingine ni yule ambaye hana uvumilivu wakati wa mitihani. Isitoshe akawa ni mwenye kupakana mafuta kwa ajili ya dini yake, yuko tayari kuacha kitu chenye kuhusiana na mfumo wa Salaf, huyu hana lolote kuhusiana na mfumo wa Salaf. Kinachozingatiwa sio madai matupu, kinachozingatiwa ni uhalisia.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: as-Salafiyyah haqiyqatuhaa wa simaatuhaa, uk. 18-20
- Imechapishwa: 06/05/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)