04. Haki juu ya sifa za Allaah inatakiwa kukubaliwa kutoka kwa viumbe wote

4- ´Aliy bin Muhammad bin al-Hasan na Ahmad bin Hamdaan ash-Shaarikiy wametuhadithia: Haamid bin Muhammad ametuhadithia: Abuu Muslim ametuhadithia: Abuu ´Aaswim ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan ath-Thawriy, kutoka kwa Manswuur, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Abiydah, kutoka kwa ´Abdullaah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesema:

“Kuna jirani katika watu wa Kitabu aliyekuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema: “Ee Muhammad! Hakika Allaah (Ta´ala) ataziweka mbingu kwenye kidole, ardhi kwenye kidole, milima kwenye kidole na udongo kwenye kidole. Halafu atasema: “Mimi ndiye Mfalme!” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akacheka mpaka magego yake yakaonekana. Kisha akasoma:

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ

“Hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria na hali ardhi yote itakamatwa mkononi Mwake siku ya Qiyaamah na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kulia.” (39:67)

Fudhwayl na Shaybah wameongeza:

“Alicheka kwa ajili ya kushangazwa na kumsadikisha.”[1]

[1] al-Bukhaariy (7414) na Muslim (2786).

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 25
  • Imechapishwa: 08/01/2017