13 – Ishaaq bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Ibn-ul-Mubaarak ametuhadithia, kutoka kwa Yahyaa bin Ayyuub, kutoka kwa ´Ubaydullaah bin Zahr, kutoka kwa ´Aliy bin Yaziyd, kutoka kwa al-Qaasim, kutoka kwa Abu Umaamah, ambaye ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Allaah amesema: “Hakika walii wangu bora zaidi ni muumini aliye na pesa kidogo lakini anayo sehemu ya swalah. Anaifanya uzuri ´ibaadah ya Mola wake, anamtii kwa faragha na akawa hafahamiki miongoni mwa watu na wala haonyeshwi kwa vidole. Ni nani mwenye kuvumilia juu ya hayo?” Kisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaonyesha kwa mkono wake na kusema: “Kifo chake huja mapema, urithi wake ni mchache na waombolezaji wake ni wachache.”[1]
14 – Ishaaq ametuhadithia: ´Aamir bin Yasaaf ametuhadithia, kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr, ambaye ameeleza kuwa ´Abdullaah bin Mas´uud amesema:
“Kuweni chemchem za elimu, wenye nyoyo mpya, nguo chakavu na taa za usiku, ili mjulikane kwa watu wa mbinguni na mjifiche kwa watu wa ardhini.”
15 – Muhammad bin ´Aliy bin al-Hasan ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin ´Alqamah ametuhadithia: Hazm ametuhadithia: Nimemsikia Mu´aawiyah bin Qurrah akisema: Ka´b amesema:
“Twubaa kwao! Twubaa kwao!” Kukasemwa: “Ni kina nani hao, ee Abu Ishaaq?” Akasema: “Twubaa kwao! Ni watu ambao wanapoomba, hawaachwi kuingia ndani. Wanapochumbia, hawaozeshwi. Wanapotembea, hawakosekani.”
16 – Muhammad bin ´Aliy ametuhadithia: Nimemsikia baba yangu akisema: Muhammad bin Muslim at-Twaa-ifiy ametuhadithia: ´Uthmaan bin ´Abdillaah bin Aws ametuhadithia, kutoka kwa Sulaym bin Hurmuz, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr, ambaye amesema:
“Waja wa Allaah wanaopendwa zaidi na Allaah ni wageni.” Akaulizwa: “Ni kina nani wageni?” Akasema: “Ni wale wanaokimbia na dini yao. Watakusanywa siku ya Qiyaamah pamoja na ´Iysaa bin Maryam (´alayhis-Salaam).”
17 – Muhammad bin ´Aliy bin Shaqiyq ametuhadithia: Ibraahiym bin al-Ash´ath ametuhadithia: Nimemsikia al-Fudhwayl akisema:
”Nimefikiwa na khabari kwamba Allaah (Ta´ala) atamwambia mja Wake juu ya baadhi ya neema Zake alizomneemesha: “Je, Sikukuneemesha? Je, Sikukupa? Je, Sikukustiri? Je, sikufanya, nikafanya, nikafanya? Sikunyamazishia sifa yako?”
Nikamsikia akisema:
“Ukiweza kutojulikana, basi fanya hivyo. Ni kipi kinachokudhuru usipotambulika? Ni kipi kinachokudhuru usiposifiwa? Ni kipi kinachokudhuru ukisemwa vibaya mbele za watu ikiwa unasifiwa mbele ya Allaah (´Azza wa Jall)?”
18 – ´Abdullaah bin Wadhdhwaah amenihadithia: Yahyaa bin Yamaan amenihadithia, kutoka kwa ´Abdul-Waahid bin Muusaa: Nimemsikia Ibn Muhayriyz akisema:
“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba ukumbusho uliositirika!”
19 – Muhammad bin al-Husayn amenihadithia: Yahyaa bin Abiy Bukayr ametuhadithia: Ismaa´iyl bin ´Ayyaash ametuhadithia: Yahyaa bin Abiy ´Amr as-Saybaaniy ametuhadithia: Mtu mmoja aliyemsikia Ka´b amenihadithia kuwa amesema:
“Hakika mimi nimekuta ndani ya Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall) sifa ya watu fulani ambao sijawaona bado; nywele zao ni timtim na nguo chafu. Wakichumbia wanawake hawaozwi. Wakihudhuria milangoni hawaruhusiwi kuingia. Haja ya mmoja wao huzunguka kwenye kifua chake. Lau nuru yake mmoja wao siku ya Qiyaamah ingegawanywa kwa viumbe wote ingewatosha.”
[1] at-Tirmidhiy (2347), ambaye amesema kuwa ni nzuri, na al-Haakim (4/123), ambaye amesema kuwa cheni ya wapokezi ni Swahiyh ambapo adh-Dhahabiy ameona kuwa ni dhaifu. Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (2347).
- Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 37-45
- Imechapishwa: 21/01/2026

Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 37-45
Imechapishwa: 21/01/2026
https://firqatunnajia.com/04-baki-kutokujulikana/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket