03. Waliposhindwa kumkabili Ibn Taymiyyah kwa hoja na dalili

Kutokana na ´Aqiydah hii Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) alitoa jawabu lake katika kitabu hiki. Ilikuwa mwaka wa 698. Wakati lilipodhihiri jibu hili kulitokea majanga na mitihani; alihukumiwa, akafungwa na kutwezwa. Shaykh alipewa mitihani na kuhukumiwa. Wakati walishindwa kumshinda kwa dalili na hoja, wakamtia gerezani kwa sababu ya jawabu hili na kwa sababu ya jawabu lake la kuyatembelea makaburi. Anayo fatwa ambayo anakataza kufunga safari kwa ajili ya kuyatembelea makaburi. Walimshambulia na wakamfanyia ukali, kwa sababu wao walikuwa wanaona kufaa kuyafungia safari makaburi. Kwa sababu wao ni waabudia makaburi na makuba ilihali yeye anafunga njia dhidi yao. Wakamsingizia kuwa eti anawatukana mawalii na waja wema. Yote hayo kwa sababu ya jibu hili. Himdi zote anastahiki Allaah hawakufuzu kwa chochote. Walitwezeka na kudhalilika. Haki ikashinda ilihali ni wenye kuchukia na himdi zote ni stahiki ya Allaah.

Ni jawabu lenye manufaa sana kwa sababu limebeba kanuni kuu zinazoweza kumfaa mwanafunzi.

Jengine ni kwamba tunapata faida kuwa wanazuoni ndio ambao wanatakiwa kurejelewa kunako maswali na mambo yenye kutatiza mbalimbali. Hawatakiwi kurejelewa wajinga na watu wanaojifanya kuwa ni wanazuoni. Wala hawatakiwi kurejelewa wapotofu na watu waliopinda. Wanatakiwa kurejelewa watu wenye uwezo wa kukagua na umaizi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 25-26
  • Imechapishwa: 23/07/2024