2 – Abiyl-Hasan ´Aliy bin Ahmad bin Muhammad bin Daawuud ar-Razzaaz ametukhabarisha: ´Aliy bin Ibraahiym bin Hammaad al-Answaariy ametukhabarisha: al-Mufadhdhwal bin Muhammad al-Janadiy ametukhabarisha: Swaamit bin Mu´aadh al-Janadiy ametuhadithia: ´Abdul-Majiyd bin ´Abdil-´Aziyz bin Abiy Rawwaad ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan ath-Thawriy, kutoka kwa Swafwaan bin Sulaym, kutoka kwa ´Adiy bin ´Adiy, kutoka kwa as-Swunaabihiy, kutoka kwa Mu´aadh bin Jabal, aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Haitovuka miguu ya mja siku ya Qiyaamah mpaka aulizwe juu ya mambo manne: umri wake aliuteketeza katika mambo gani, mali yake aliipata kivipi na akaitumia wapi na elimu yake aliifanyisha nini.”[1]
3 – Abul-Husayn ´Aliy bin ´Abdil-Wahhaab bin Ahmad bin Muhammad as-Sukkariy ametukhabarisha: Abu ´Umar Muhammad bin al-´Abbaas al-Khazzaaz ametuhadithia: Abu Muhammad Ja´far bin Ahmad al-Marwaziy al-Mu-adhdhin ametukhabarisha: Ismaa´iyl bin Muhammad bin Yahyaa bin Hammaad bin Habiyb bin Sa´d, mtumwa wa al-Fadhwl bin al-´Abbaas bin ´Abdil-Malik Kuufah, ametuhadithia: Ibn Fudhwayl ametuhadithia, kutoka kwa Layth, kutoka kwa ´Adiy bin ´Adiy, kutoka kwa Rajaa’ bin Hayawah, kutoka kwa Mu´aadh bin Jabal, ambaye amesema:
“Haitovuka miguu ya mja siku ya Qiyaamah mpaka aulizwe juu ya mambo manne: mwili wake aliutumia vipi, umri wake aliuteketeza katika mambo gani, mali yake aliipata kivipi na akaitumia wapi na elimu yake aliifanyisha nini.”[2]
4 – Abul-Husayn Muhammad bin al-Hasan bin Ahmad al-Ahwaaziy ametukhabarisha: Muhammad bin Ishaaq bin Ibraahiym al-Qaadhwiy ametuhadithia huko Ahwaz: Muhammad bin ´Abdus al-Kaatib ametuhadithia: Zayd bin al-Harash ametuhadithia: ´Abdullaah bin Khiraash, kutoka kwa al-´Awwaam, kutoka kwa Abu Swaadiq, kutoka kwa ´Aliy, aliyesema:
”Bwana mmoja alisema: ”Ee Mtume wa Allaah, ni kipi kinachoniondoshea hoja ya ujinga?” Akasema: ”Elimu.” Akasema: ”Ni kipi kinachoniondoshea hoja ya elimu?” Akasema: ”Matendo.”[3]
5 – Abul-Fath Muhammad bin Ahmad bin Abiyl-Fawaaris al-Haafidhw, Abu Bakr Muhammad bin Ahmad bin Yuusuf as-Swayyaad na Abu ´Aliy al-Hasan bin Ahmad bin Ibraahiym bin Shaadhaan wametukhabarisha: Abu Bakr Ahmad bin Yuusuf bin Khallaad an-Naswiybiy ametukhabarisha: al-Haarith bin Muhammad bin Abiy Usaamah ametukhabarisha: al-Hakam bin Muusa ametuhadithia: al-Waliyd bin Muslim ametukhabarisha, kutoka kwa Shaykh mmoja Kalb kwa kun-yah ya Abu Muhammad, aliyesimulia kuwa amemsikia Mak-huul akisimulia kutoka kwa Abud-Dardaa’, ambaye amesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinambia: ”Itakuweje, ee ´Uwaymir, ukiulizwa siku ya Qiyaamah kama ulijua au hukujua?” Ukisema kuwa ulijua, utaulizwa: ”Ulikifanyia nini kile ulichojifunza?” Na ukisema kuwa hukujua, utaulizwa: ”Nini ilikuwa udhuru wako kwa kutokujua? Ni kwa nini hukujifunza?”[4]
[1] Swahiyh kupitia ile iliyotangulia. al-Mundhiriy amesema katika “at-Targhiyb wat-Tarhiyb”:
”Ameipokea at-Twabaraaniy na al-Bazzaar kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.”
[2] Cheni yake ya wapokezi ni dhaifu. Layth bin Abiy Sulaym hajengewi hoja. Aidha ameisimulia kama maneno ya Mu´aadh. Isitoshe inatoshelezwa na zile Hadiyth mbili zilizotangulia.
[3] Cheni yake ya wapokezi ni dhaifu sana. Haafidhw Ibn Hajar amesema katika ”at-Taqriyb” ya kwamba ´Abdullaah bin Khiraash ni mnyonge. Ibn ´Ammaar amemwita kuwa ni mwongo.
[4] Cheni yake ya wapokezi ni dhaifu kwa sababu ya Shaykh Abu Muhammad al-Kalbiy, mimi simtambui ni nani. Isitoshe Mak-huul ni mwenye hadhaa, hakutamka wazi amesikia kutoka kwa nani.
- Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 17-19
- Imechapishwa: 06/05/2024
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)