Uhakika wa furaha ni ile raha, utulivu, amani na furaha inayopatikana moyoni na kuondokewa na dhiki na hamu na mtu kuhisi starehe na yule anayeshirikiana naye katika maisha ya nyumbani kwake.
Hakika furaha ina sababu na milango. Tutajaribu katika usiku huu kulenga baadhi ya sababu zake na kuifungua baadhi ya milango yake. Hakuna kilichotupelekea kufanya hivo na kuzungumzia kuhusu furaha ya familia katika zama hizi ambapo kumejaa upuuzi na amekuwa kila mmoja katika familia ni mwenye kujifungia katika ulimwengu wake maalum. Intaneti zimevamia majumba yetu na imekuwa baadhi ya wanandoa wanajifungia kwenye vyumba vyao wakiangalia kitu hichi na wakati huo huo watoto wanajitenga mbali na wazazi wao wakiangalia kitu hichi.
Kuna wengine wanajifungia wenyewe wakiangalia chaneli. Utakuta mmoja anaangalia chaneli fulani, mwingine haitaki chaneli hiyo na hivyo ananunua TV nyingine na kadhalika. Wanafamilia wamekuwa mbalimbali ilihali wote wamo katika nyumba moja, sembuse jamii kwa jumla. Wengi wetu tumekuwa wenye kuhisi ugeni majumbani mwetu na mafungamano kati ya wanandoa wao kwa wao, mafungamano ya wazazi na watoto, mafungamano ya watoto na wazazi na mafungamano ya ndugu wao kwa wao yamekuwa si mazuri. Haya ndio yametufanya kuzungumzia sababu ya familia kupata furaha.
- Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Asbaab sa´aadat-il-Usrah, uk. 15-16
- Imechapishwa: 08/10/2016
Uhakika wa furaha ni ile raha, utulivu, amani na furaha inayopatikana moyoni na kuondokewa na dhiki na hamu na mtu kuhisi starehe na yule anayeshirikiana naye katika maisha ya nyumbani kwake.
Hakika furaha ina sababu na milango. Tutajaribu katika usiku huu kulenga baadhi ya sababu zake na kuifungua baadhi ya milango yake. Hakuna kilichotupelekea kufanya hivo na kuzungumzia kuhusu furaha ya familia katika zama hizi ambapo kumejaa upuuzi na amekuwa kila mmoja katika familia ni mwenye kujifungia katika ulimwengu wake maalum. Intaneti zimevamia majumba yetu na imekuwa baadhi ya wanandoa wanajifungia kwenye vyumba vyao wakiangalia kitu hichi na wakati huo huo watoto wanajitenga mbali na wazazi wao wakiangalia kitu hichi.
Kuna wengine wanajifungia wenyewe wakiangalia chaneli. Utakuta mmoja anaangalia chaneli fulani, mwingine haitaki chaneli hiyo na hivyo ananunua TV nyingine na kadhalika. Wanafamilia wamekuwa mbalimbali ilihali wote wamo katika nyumba moja, sembuse jamii kwa jumla. Wengi wetu tumekuwa wenye kuhisi ugeni majumbani mwetu na mafungamano kati ya wanandoa wao kwa wao, mafungamano ya wazazi na watoto, mafungamano ya watoto na wazazi na mafungamano ya ndugu wao kwa wao yamekuwa si mazuri. Haya ndio yametufanya kuzungumzia sababu ya familia kupata furaha.
Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Asbaab sa´aadat-il-Usrah, uk. 15-16
Imechapishwa: 08/10/2016
https://firqatunnajia.com/03-uhakika-wa-furaha-katika-familia/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)