Miongoni mwa jumla ya maimamu hawa ambao waliandika ´Aqiydah ya Salaf ni pamoja vilevile na Imaam Abu Ja´far Ahmad bin Muhammad bin Salaamah al-Azdiy at-Twahaawiy. Alikuwa ni miongoni mwa wanachuoni wa karne ya 300 huko Misri. Amenasibishwa na mji mmoja unaoitwa Twahaa huko Misri. Ameandika kitabu hiki kifupi, chenye manufaa na faida.

Kimeandikiwa vitabu vingi vinavyokifafanua, takriban vitabu saba. Hata hivyo vyote vina makosa. Kwa sababu wale walioviandika wana mfumo wa karne hizi zilizokuja nyuma. Kwa ajili hiyo maelezo yao hayakusalimika na makosa na kwenda kombo na yale yaliyomo katika ´Aqiydah ya at-Twahaawiy. Kutokana na vile tunavyojua kuna ufafanuzi mmoja uliosalimika; ufafanuzi wa Ibn ´Abdil-´Izz, ambao pia unaitwa “Sharh at-Twahaawiyyah”. Kutokana na inavyodhihiri ni kwamba mwanachuoni huyu alikuwa katika wanafunzi wa Ibn Kathiyr. Maelezo yake haya kuna nukuu nyingi kutoka katika vitabu vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, vitabu vya Ibn-ul-Qayyim na vitabu vya maimamu wengine. Ni kitabu kikubwa. Wanachuoni walikuwa wakikirejelea na wakikitilia umuhimu kutokana elimu yake na usahihi wa maaluumaat yaliyomo. Kwa hivyo ni kitabu kitukufu na ni marejeo makubwa katika marejeo ya ´Aqiydah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 26-27
  • Imechapishwa: 04/06/2019