Tofauti ya Salaf juu ya tafsiri ni ndogo. Tofauti yao katika hukumu ni kubwa zaidi kuliko tofauti zao kuhusiana na tafsiri. Jengine ni kwamba tofauti nyingi zinazosihi kutoka kwao zinahuziana na tafauti ya sampuli na si tofauti za kupingana. Tofauti hizo ni aina mbili:

1 – Watu wawili wanaelezea matakwa yao kwa matamshi mawili tofauti. Maana ya kitu cha kwanza si maana ya kitu cha pili. Hata hivyo kitu hicho kilichopewa jina ni kimoja, kama ilivyo hali ya majina yanayofanana ambayo yako kati ya maneno yenye maana sawa na yale yenye maana tofauti kabisa. Ni kama yalivyo majina tofauti ya upanga, majina mazuri ya Allaah, majina ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na majina ya Qur-aan. Hakika majina ya Allaah yote yanafahamisha mwitwaji mmoja. Kwa hivyo kumuomba kwa jina moja miongoni mwa majina Yake mazuri hakupingani na kumwomba kwa jina jingine. Bali hali ni kama alivosema Allaah:

قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖأَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ

“Sema: “Muiteni Allaah au muiteni Mwingi wa rehema! Vyovyote mtakavyomwita [bado ni Yuleyule Mmoja], Yeye ana majina mazuri kabisa.”[1]

Kila moja ya majina Yake yanafahamisha juu ya dhati ya mwitwaji na sifa iliyobebwa na jina hilo. Mjuzi wa yote linafahamisha dhati na ujuzi, Muweza linafahamisha dhati na uwezo, Mwingi wa rehema linafahamisha dhati na rehema. Yule mwenye kudai kwamba anashikamana na dhahiri na huku anapinga kwamba majina Yake yanajulisha sifa Zake anazungumza kwa mujibu wa imani ya Baatwiniyyah wa Qarraamiyyah ambao wanasema kuwa haitakiwi kusema kuwa Yuko hai wala kwamba Hayuko hai. Wanapinga Kwake mambo mawili yanayopingana kwa wakati mmoja. Qarraamiyyah wa Baatwiyyah hawapingi jina lenyewe kama lenyewe, isipokuwa zile sifa zilizobebwa na majina. Yeyote anayeafikiana na ajenda ya Baatwiyyah waliochupa mipaka, ingawa atadai udhahiri uliochupa mipaka, basi atakuwe pia ameenda sambamba na ´Aqiydah yao katika jambo hili. Hili si muhimu hivi sasa. Hata hivyo kilicho muhimu kwa sasa ni kwamba kila jina miongoni mwa majina Yake linafahamisha dhati Yake, kwamba majina Yake yanafahamisha sifa Zake na kwamba sifa Zake pia zinafahamisha majina Yake mengine.

Kinachofaa, hata hivyo, ni kwamba majina Yake yote yanaonyesha dhati Yake, kwamba majina Yake yanaonyesha sifa Zake, na kwamba sifa Zake pia zinaonyeshwa katika majina Yake mengine.

Vilevile inaweza kusemwa kuhusu majina ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), kama vile Muhammad, Mtokomezaji (الماحي), Mkusanyaji (الحاشر) na wa Mwisho (العقيب).

Vivyo hivyo kuhusu majina ya Qur-aan, kama vile Upambanuzi (الفرقان), Mwongozo (الهدى), Tiba (الشفاء), Ubainifu (البيان) na Kitabu (الكتاب).

Kwa hivyo ikiwa muulizaji anakusudia kitu kilichopewa jina, basi tutamjibu kwa kila jina ambalo anatambulika kwalo mwitwaji. Jina hilo linaweza kuwa jina lenyewe na linaweza kuwa sifa. Mfano wa hilo ni ambaye anauliza kuhusu maneno Yake (Ta´ala):

وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا

”Atakayepuuza ukumbusho Wangu, basi hakika atapata maisha ya dhiki.”[2]

Ukumbusho wake ni upi? Ni Qur-aan na pengine vilevile ikawa ni vile vitabu Vyake alivyoteremsha. Kwa sababu ukumbusho (الذكر) ni kitenzi na kwa hivyo inaweza kuambatishwa kwa mtenda kitendo au kwa kitendo chenyewe. Kwa hivyo ikisemwa ukumbusho wa Allaah kwa maana ya pili, basi ina maana ya yale ambayo mja anamtaja Allaah kwayo:

سبحان الله و الحمد لله و لا إله إلا الله و الله أكبر

”Allaah ametakasika na mapungufu, Allaah ni mkubwa, hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na Allaah ni mkubwa.”

Na tukisema ukumbusho wa Allaah kunakusudiwa mtenda kitendo, nacho ni kile Anachokisema, nayo ni yale maneno Yake. Hayo ndio makusudio ya maneno Yake (Ta´ala):

وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا

”Atakayepuuza ukumbusho Wangu, basi hakika atapata maisha ya dhiki.”

Kwa sababu kabla ya hapo Amesema:

فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَىٰ ٰ

”Utakapokufikieni kutoka Kwangu uongofu, basi atakayefuata uongofu Wangu hatopotea na wala hatopata mashaka.”[3]

Uwongofu wake ni yale Anayoyateremsha katika ukumbusho. Lengo ni kutambua ya kwamba ukumbusho ni yale maneno Yake yaliyoteremshwa au kule mja kumtaja. Ni mamoja itasemwa ukumbusho Wangu Kitabu Changu, maneno Yangu au mwongozo Wangu, basi kunakusudiwa kitu kimoja.

Ikiwa malengo ya muulizaji ni kujua sifa maalum inayohusiana na jina fulani, basi ni lazima kuongeza ufafanuzi juu ya kutaja jina hilo. Kwa mfano aulize kuhusu Aayah:

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ

”Yeye ni Allaah, ambaye hakuna mungu wa haki isipokuwa Yeye, mfalme, mtakatifu, Mwenye kusalimisha na kusalimika, Mwenye kusadikisha ahadi na kuaminisha, Mwenye kudhibiti, kushuhudia, kuchunga na kuhifadhi, Mwenye nguvu zisizoshindwa, Jabari, Mwenye ukubwa na utukufu.”[4]

Amejua kuwa mkusudiwa ni Allaah, lakini anataka anachotaka kujua ni nini maana ya kwamba Yeye ni ”Mwenye kusalimisha na kusalimika, Mwenye kusadikisha ahadi na kuaminisha”.

Kwa hivyo inapofahamika hili tunaona kwamba Salaf mara nyingi walikuwa wakielezea kile kinachoitwa kwa namna inayokifahamisha ingawa namna hiyo inayo sifa isiyopatikana katika jina jingine. Kama mfano wa mtu kusema kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye Mkusanyaji (الحاشر), Mtokomezaji (الماحي) na wa Mwisho (العقيب) na kwamba Mtakatifu ndiye Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. Kwa maana nyingine mwitwaji ni mmoja na yuleyule, haimaanishi kwamba sifa moja ni sawa na nyingine. Hiyo sio tofauti ya kupingana, kama wanavyofikiri baadhi ya watu. Mfano wa hilo ni tafsiri yao kwamba Njia iliyonyooka kwa mujibu wa baadhi yao ni Qur-aan, kwa maana wale wenye kuifuata. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ndio kamba ya Allaah madhubuti, ukumbusho wenye hekima na njia ilionyooka.”[5]

Ameipokea at-Tirmidhiy na Abu Nu´aym kupitia njia nyingi.

Baadhi ya wengine wakasema kwamnba ni Uislamu, at-Tirmidhiy na wengineo wamepokea kupitia kwa an-Nawwaas bin Sam´aan kwamba yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah ametoa mfano wa njia iliyonyooka. Kando ya njia hiyo kuna kuta mbili. Katika hizo kuta kuna milango iliyo wazi. Kwenye milango hiyo kuna mapazia yaliyoteremshwa. Kuna mlinganizi anayeita kutoka juu ya njia hiyo, mlinganizi mwingine yuko mwanzoni mwa njia hiyo. Njia iliyonyooka ni Uislamu, kuta hizo mbili ni mipaka ya Allaah, milango iliyo wazi ni yale mambo aliyoyaharamisha Allaah, mlinganizi aliye mwanzoni mwa njia ni Kitabu cha Allaah, mlinganzi aliye juu ya njia ni mwonyaji wa Allaah katika moyo wa kila muumini.”[6]

Maoni haya mawili yanaafikiana, kwa sababu Uislamu ni kufuata Qur-aan, lakini kila mmoja katika wao ametoa maelezo kwa njia inayotofautiana na mwenzake. Ni kama ambavyo neno “njia ilionyooka” linaweza kutolewa maelezo kwa njia nyingine ya tatu; Sunnah na Mkusanyiko, utumwa, kumtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mfano wa hayo. Kwa hivyo maono yote haya yameashiria kitu kimoja, lakini kwa namna tofauti tofauti.

[1] 17:110

[2] 20:124

[3] 20:123-126

[4] 59:23-24

[5] at-Tirmidhiy (2906), ambaye amesema kuwa ni nzuri na ngeni. Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (2906).

[6] at-Tirmidhiy (2859), ambaye amesema kuwa ni nzuri na ngeni. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (2859).

  • Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 24-31
  • Imechapishwa: 20/03/2025