يَوْمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ امْتَلَأْتِ وَتَقُولُ هَلْ مِن مَّزِيدٍ
“Siku Tutakapoiambia Jahannam: “Je, umeshajaa?” Nayo itasema: “Je, hakuna ziada yoyote?”
Mtume (Swalla Allâhu ´alayhi wa sallam) amesema kuwa Allaah (´Azza wa Jall) ataweka unyayo Wake, ambapo useme: ”Tosha, tosha”
9 – Muhammad bin al-Husayn bin al-Hasan al-Qattwaan ametukhabarisha huko Naysaabuur: Ahmad bin Yuusuf as-Sulamiy ametuhadithia: ´Abdur-Razzaaq ametuhadithia: Ma´mar ametuhadithia, kutoka kwa Hammaam bin Munabbih: Haya ndio yale ambayo Abu Hurayrah ametusimulia kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Pepo na Moto vilizozana ambapo Moto ukasema: “Ndani yangu wanaingia wakandamizaji na wenye kiburi.” Pepo nayo ikasema: “Ndani yangu wanaingia watu wadhaifu na wale watu duni.” Ndipo Akasema (´Azza wa Jall) kuuambia Moto: “Wewe ni adhabu Yangu ambayo namuadhibu Nimtakaye katika waja Wangu.” Akasema kuiambia Pepo: “Wewe ni huruma Yangu ambayo Namrehemu kwayo Nimtakaye katika waja Wangu.” Kila mmoja wenu nitamjaza.” Kuhusu Moto hautojaa mpaka pale Atapoweka unyayo Wake juu yake mpaka useme: “Tosha, tosha.” Hapo ndipo utajaa na ujikusanye.” Hapo ndipo utajaa na ujikusanye. Allaah (´Azza wa Jall) hamdhulumu yeyote katika viumbe Wake. Kuhusu Pepo, Allaah (´Azza wa Jall) atauumbia viumbe.”
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Allaah amemuumba Aadam kwa sura Yake. Urefu wake ilikuwa dhiraa sitini. Baada ya Kumuumba akasema: ”Nenda na uwasalimie wale kule. Huko kulikuwepo kundi la Malaika wameketi. Usikilize watakusalimia vipi, kwani hakika hiyo ndio yatakuwa mamkizi yako na mamkizi ya kizazi chako.” Akawaendea na kusema:
السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ
”Amani ya Allaah iwe juu yenu.”
Wakajibu:
و عليك السلام و رحمة الله
”Nawe amani na rehema ya Allaah iwe juu yako.”
[Wakazidisha ”rehema ya Allaah”]. Kila ambaye ataingia Peponi atakuwa na umbile la Aadam na urefu wake itakuwa dhiraa sitini. Baada ya hapo umbile la watu litapungua mpaka sasa.”
Hadiyth hii ni yenye kuthibiti kwa maafikiano ya wale mabingwa.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 41-42
- Imechapishwa: 08/06/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 41-42
Imechapishwa: 08/06/2026
https://firqatunnajia.com/03-pindi-allaah-atakapoweka-unyayo-wake-juu-ya-moto/