3 – Abu Muusa al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayi wa sallam) amesema:

“Mfano wa yule ambaye anamtaja Mola wake na ambaye hamtaji Mola wake ni kama mfano wa aliye hai na maiti.”[1]

Kuna maafikiano juu yake.

Imekuja katika tamko la Muslim:

“Mfano wa nyumba ambayo Allaah hutajwa ndani yake na nyumba ambayo Allaah hatajwi ndani yake, ni kama mfano wa aliye hai na maiti.”

MAELEZO

Hadiyth hii inahimiza dhikr kwa jumla, ni mamoja dhikr hizo ni kusoma Qur-aan, kuswali, kuomba du´aa, kusema “Subhaan Allaah”, kusoma vitabu vya wanazuoni na kusoma vitabu vya ´Aqiydah. Yote hayo ni katika kufanya dhikr. Kwa hivyo muislamu anatakiwa kuwa mwenye kumtaja Allaah ili asiwe maiti. Uzembe na mfano wake kunaidumaza akili na mwenye kumtaja Allaah anakuwa hai.

[1] al-Bukhaariy (6407) na Muslim (779).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 09
  • Imechapishwa: 24/09/2025