2 – Kusherekea maulidi ni kitu kilichozuliwa na Shiy´ah Faatwimiyyuun baada ya karne bora kwa lengo la kuiharibu dini ya waislamu. Mwenye kufanya kitu kwa nia ya kujikurubisha kwa Allaah (Ta´ala) na kitu hicho kikawa hakikufanywa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hakukiamrisha na wala hakikufanywa na makhaliyfah wake baada yake, basi kitendo chake ni kumtuhumu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa hakuwabainishia watu dini yao. Isitoshe vilevile jengine ni kuyakadhibisha maneno Yake Allaah (Ta´ala):

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ

”Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema Yangu.”[1]

Hilo ni kwa sababu amekuja na jipya ambalo anadai kuwa ni sehemu katika dini ilihali halikuleta Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] 05:03

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huquwq-un-Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bayn al-Ijlaal wal-Ikhlaal, uk. 150
  • Imechapishwa: 06/09/2025