02. Maulidi si katika mwenendo wa Mtume wala Maswahabah wake

Kusherehekea maulidi sio katika Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala sio Sunnah ya makhaliyfah wake. Kusherehekea maulidi kwa mnasaba wa kuzaliwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kitu kimechokatazwa na kurudishwa kwa njia nyingi:

1 – Haikuwa katika Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala makhaliyfah wake. Mambo yakishakuwa hivyo, basi ni katika Bid´ah iliyokatazwa. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Jilazimisheni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu na wenye kuongoza baada yangu. Shikamaneni nazo barabara na ziumeni kwa magego yenu. Tahadharini na mambo ya kuzua! Hakika kila kitachozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”[1]

[1] Ahmad (16692) at-Tirmidhiy (2676).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huquwq-un-Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bayn al-Ijlaal wal-Ikhlaal, uk. 149
  • Imechapishwa: 06/09/2025