10 – Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Je, nisikujuze maneno yanayopendeza zaidi kwa Allaah?” Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah, nijuze maneno yanayopendeza zaidi kwa Allaah.” Akasema: “Hakika maneno yanayopendeza zaidi kwa Allaah ni:
سُبْحَانَ اللَّهِ وَبِحَمْدِهِ
“Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu na himdi zote ni Zake.”
Imekuja katika tamko jengine:
“Hakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa: “Ni maneno yepi bora?” Akajibu:
“Yale ambayo Allaah amewachagulia Malaika au waja Wake:
سُبْحَانَ اللَّهِ وَبِحَمْدِهِ
“Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu na himdi zote ni Zake.”[1]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Hadiyth inamthibitishia Allaah ´Azza wa Jall) mapenzi, tofauti na wale walioyapinga. Allaah (´Azza wa Jall) anasifiwa mapenzi, mapenzi ya hali ya juu (الخلة) na upendo.
Kinachokusudiwa ni maneno ya watu yanayopendeza zaidi kwa Allaah. Ama kwa kuachia maneno ya Allaah (´Azza wa Jall) ndio yanayopendeza zaidi Kwake. Kusoma Qur-aan ni bora zaidi kuliko kusema “Subhaan Allaah” na “Alhamdulillaah”. Hata hivyo dhikr zilizofungamanishwa – kama vile adhkaar za asubuhi na jioni na kumuitikia muadhini – zinafanywa katika wakati wake, kwa sababu zinakwisha kwa kumalizika wakati wake. Kwa msemo mwingine yule msomaji atasimama na hatozileta tena. Kanuni inasema kuwa ikiwa dhikr imewekewa wakati maalum basi inatangulizwa mbele ya usomaji wa Qur-aan. Kwa sababu dhikr zilizowekewa wakati zinakwisha kwa kumalizika wakati wake.
[1] Muslim (2731).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 18
- Imechapishwa: 28/09/2025
10 – Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Je, nisikujuze maneno yanayopendeza zaidi kwa Allaah?” Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah, nijuze maneno yanayopendeza zaidi kwa Allaah.” Akasema: “Hakika maneno yanayopendeza zaidi kwa Allaah ni:
سُبْحَانَ اللَّهِ وَبِحَمْدِهِ
“Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu na himdi zote ni Zake.”
Imekuja katika tamko jengine:
“Hakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa: “Ni maneno yepi bora?” Akajibu:
“Yale ambayo Allaah amewachagulia Malaika au waja Wake:
سُبْحَانَ اللَّهِ وَبِحَمْدِهِ
“Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu na himdi zote ni Zake.”[1]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Hadiyth inamthibitishia Allaah ´Azza wa Jall) mapenzi, tofauti na wale walioyapinga. Allaah (´Azza wa Jall) anasifiwa mapenzi, mapenzi ya hali ya juu (الخلة) na upendo.
Kinachokusudiwa ni maneno ya watu yanayopendeza zaidi kwa Allaah. Ama kwa kuachia maneno ya Allaah (´Azza wa Jall) ndio yanayopendeza zaidi Kwake. Kusoma Qur-aan ni bora zaidi kuliko kusema “Subhaan Allaah” na “Alhamdulillaah”. Hata hivyo dhikr zilizofungamanishwa – kama vile adhkaar za asubuhi na jioni na kumuitikia muadhini – zinafanywa katika wakati wake, kwa sababu zinakwisha kwa kumalizika wakati wake. Kwa msemo mwingine yule msomaji atasimama na hatozileta tena. Kanuni inasema kuwa ikiwa dhikr imewekewa wakati maalum basi inatangulizwa mbele ya usomaji wa Qur-aan. Kwa sababu dhikr zilizowekewa wakati zinakwisha kwa kumalizika wakati wake.
[1] Muslim (2731).
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 18
Imechapishwa: 28/09/2025
https://firqatunnajia.com/03-maneno-yanayopendeza-zaidi-kwa-allaah/