9 – ´Aliy bin ´Abdillaah ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa ´Umaarah bin al-Qa´qaa´, kutoka kwa Abu Zur´ah, kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesema:

”Bwana mmoja alisema: ”Ee Mtume wa Allaah! Ni mtu gani anayestahiki zaidi matangamano mazuri?” Akasema: ”Mama yako.” Akasema: ”Kisha anafuatia nani?” Akasema: ”Kisha mama yako.” Akasema: ”Kisha anafuatia nani?” Akasema: ”Baba yako.”

Wanaona kuwa mama yako ana haki ya kupewa theluthi mbili na baba yako ana haki ya theluthi moja.

Kulisemwa kuambiwa Sufyaan:

”Mama anayo haki ya kupewa theluthi mbili katika Hadiyth?” Akasema: ”Ndio. Nimeisikia kutoka kwa Ibn Shubrumah, ambaye ameisimulia kutoka kwa ´Umarah kabla ya kumuona. Nikamuuliza ´Umaarah, ndipo akaifikisha.”

10 – Qutaybah ametuhadithia: Jariyr ametuhadithia, kutoka kwa ´Umaarah bin Shubrumah, kutoka kwa Abu Zur´ah, kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesema:

”Bwana mmoja alisema: ”Ee Mtume wa Allaah! Ni mtu gani anayestahiki zaidi matangamano mazuri?” Akasema: ”Mama yako.” Akasema: ”Kisha anafuatia nani?” Akasema: ”Kisha mama yako.” Akasema: ”Kisha anafuatia nani?” Akasema: ”Mama yako.” Akasema: ”Kisha anafuatia nani?” Akasema: ”Baba yako.”

11 – Sulaymaan bin Harb ametuhadithia: Wuhayb bin Khaalid ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Shubrumah: Nimemsikia Abu Zur´ah, kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesema:

”Kulisemwa: ”Ee Mtume wa Allaah! Nimtendee wema nani?” Akasema: ”Mama yako.” Akasema: ”Kisha anafuatia nani?” Akasema: ”Kisha mama yako.” Akasema: ”Kisha anafuatia nani?” Akasema: ”Kisha mama yako.” Akasema: ”Kisha anafuatia nani?” Akasema: ”Baba yako.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 110-111
  • Imechapishwa: 16/12/2024

Turn on/off menu