Madhambi yanapelekea katika upweke ambao anahisi yule mtenda dhambi kati yake yeye na Allaah. Ndani yake hakuna utamu wowote ule kabisa. Iwapo atapata utamu wa ulimwenguni kote, basi utamu huo usingefaa chochote kwa upweke huo. Hili ni jambo ambalo hakuna anayelihisi isipokuwa yule ambaye moyoni mwake kuna uhai. Kwani mfu hahisi maumivu yoyote kwa donda. Lau mtu angeliacha madhambi kwa sababu ya kuepuka upweke huo, basi ingelitosha kwa yule mwenye busara kuyaepuka. Hakuna kitu kinachofanya moyo kuwa na uchungu kama upweke wa dhambi zilizopandiana.

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 65-66
  • Imechapishwa: 28/12/2017