9 – Khalaf bin Hishaam al-Bazzaar ametuhadithia: Abu Shihaab bin al-Hannaat ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa bwana mmoja, kutoka kwa Ibn Munabbih, ambaye amesema:
“Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) alipowatuma Muusa na Haaruun kwa Fir´awn, Akasema: ”Msiogope nguo alizojipamba nazo duniani, kwani kipaji chake kiko mikononi Mwangu. Hawezi kutamka, hatingishiki wala hapumui isipokuwa kwa idhini Yangu. Wala msifurahie yale aliyopewa ulimwenguni, kwani hayo ni maua ya maisha ya dunia na mapambo ya waliopewa starehe. Lau Ningependa kuwapamba nyinyi kwa mapambo ya dunia ambayo Fir´awn akiyaona anajua kuwa hana uwezo wa kuyapata kama mlivyopewa, Ningefanya hivyo. Lakini Nawaepusha mbali na mambo hayo na Nayageuza mbali nanyi. Hivyo ndivyo Nifanyavyo kwa mawalii Wangu. Zamani kabisa Nilichagua kwa ajili yao katika mambo ya dunia. Hakika Nawakinga na neema zake kama vile mchungaji mwenye huruma anavyowakinga kondoo wake na sehemu za maangamizi. Nawapepesha mbali na starehe zake kama mchungaji mwenye huruma anavyoepusha ngamia wake sehemu chafu. Hata hivyo sifanyi hivo kwa sababu ya kuwadharau, bali ni ili wakamilishe sehemu yao ya heshima kutoka Kwangu kwa hali ya salama na ya kutoshelewa ambayo tamaa haijawadhuru na dunia haijawapunguza kwa udanganyifu wake. Hakika mawalii Wangu wanajipamba Kwangu kwa unyenyekevu, unyenyekevu, khofu na uchaji. Uchaji unathibiti nyoyoni mwao kisha huonekana miilini mwao. Hiyo ndiyo nguo yao wanayovaa, vazi lao wanalojioneshea, dhamiri yao wanayoihisi, wokovu wao wanaofanikisha kwayo, matumaini yao wanayoyategemea, utukufu wao wanaojivunia na ni alama yao wanayojulikana kwayo. Basi ukikutana nao, basi wanyenyekee kwa mabawa yako na wanyenyekee kwa moyo na ulimi wako. Fahamu ya kwamba atakayemkhofisha walii Wangu, basi amenitangazia Mimi vita na Mimi ndiye Nitakayemlipa kisasi siku ya Qiyaamah.”
10 – Rawh bin Haatim ametuhadithia: Yahyaa bin Abiy Bukayr amenihadithia, kutoka kwa Shariyk, kutoka kwa Layth, kutoka kwa al-Hakam, kutoka kwa Abul-Bakhtariy, kutoka kwa ´Aliy, ambaye amesema:
”Twubaa kwa kila mja aliyefukuzwa ambaye yeye anawajua watu lakini wao hawamjui. Allaah amemjua yeye kwa ridhaa Yake. Hao ndio taa za giza. Huzuiliwa kutoka kwao kila fitina yenye giza. Hao siyo watu wa maneno mengi wasiotafakari wala siyo watu wagumu wenye unafiki.”
Ameeleza ya kwamba amemsikia Ibn-ul-A´raabiy akisema:
“Aliyefukuzwa ni yule ambaye haingii na watu katika yale waliyomo.”
11 – ´Abdur-Rahmaan bin Swaalih ametuhadithia: Ya´laa bin ´Ubayd ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin ´Awn, kutoka kwa Ibraahiym bin ´Iysaa, kutoka kwa ´Abdullaah bin Mas´uud, aliyesema:
“Kuweni chemchemi za elimu, taa za uongofu, wakaaji wa majumbani, taa za usiku, wenye nyoyo mpya na wenye nguo zilizochakaa. Mnatambulika mbinguni na mnafichika ardhini.”
12 – Ishaaq bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Sufyaan bin ´Uyaynah ametuhadithia, kutoka kwa Abu Khaalid, aliyesimulia kwamba ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Kuweni vyombo vya Kitabu, chemchemi za elimu na muombeni Allaah riziki ya siku baada ya siku. Jihesabuni miongoni mwa wafu na wala haitokudhuruni msipotajirishwa.”
- Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 30-36
- Imechapishwa: 21/01/2026

Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 30-36
Imechapishwa: 21/01/2026
https://firqatunnajia.com/03-kuwa-si-mwenye-kutambulika-ardhini-mwenye-kutambulika-mbinguni/