2- Mikakati ya kushtua kuua viongozi wa miji kwa ajili ya kufanya uasi dhidi ya viongozi wa miji na wafalme wa Ummah na kuwaua polisi na naibu wao katika huduma za miji sio njia iliyowekwa katika Shari´ah; ni njia ya vurugu na iliyozuliwa na sura ovu ya ugaidi. Mashaytwaan wa kibinaadamu na wa kijini wanawazungumzisha magaidi kuyafanya hayo na wanawapambia ili watumbukie kwenye dhambi na tendo na jinai lililo baya. Jinai hilo linaitwa ugaidi. Hawajali kile kinachosemwa na dini, hawamuogopi mtawala, hawana haya kwa Muumba wa viumbe, hawamuhurumii kiumbe mwenye amani. Kwa kuwa wameziuza nafsi zao kwa Mashaytwaan ambao ndio wako nyuma ya chuki zote hizi kati ya watu na majini. Ni biashara mbaya iliyoje walonayo! Ni duni iliyoje matendo yao! Wameununua upotevu kwa uongofu na adhabu kwa msamaha. Hata hivyo kila jinai lina malipo yake sawasawa mbele ya Allaah:
جَزَاءً وِفَاقًا
“Malipo yanayowafikiana kabisa!”[1]
وَلَا يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا
“Mola wako hamdhulumu yeyote.”[2]
[1] 78:26
[2] 18:49
- Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Irhaab, uk. 11-12
- Imechapishwa: 02/04/2017
2- Mikakati ya kushtua kuua viongozi wa miji kwa ajili ya kufanya uasi dhidi ya viongozi wa miji na wafalme wa Ummah na kuwaua polisi na naibu wao katika huduma za miji sio njia iliyowekwa katika Shari´ah; ni njia ya vurugu na iliyozuliwa na sura ovu ya ugaidi. Mashaytwaan wa kibinaadamu na wa kijini wanawazungumzisha magaidi kuyafanya hayo na wanawapambia ili watumbukie kwenye dhambi na tendo na jinai lililo baya. Jinai hilo linaitwa ugaidi. Hawajali kile kinachosemwa na dini, hawamuogopi mtawala, hawana haya kwa Muumba wa viumbe, hawamuhurumii kiumbe mwenye amani. Kwa kuwa wameziuza nafsi zao kwa Mashaytwaan ambao ndio wako nyuma ya chuki zote hizi kati ya watu na majini. Ni biashara mbaya iliyoje walonayo! Ni duni iliyoje matendo yao! Wameununua upotevu kwa uongofu na adhabu kwa msamaha. Hata hivyo kila jinai lina malipo yake sawasawa mbele ya Allaah:
جَزَاءً وِفَاقًا
“Malipo yanayowafikiana kabisa!”[1]
وَلَا يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا
“Mola wako hamdhulumu yeyote.”[2]
[1] 78:26
[2] 18:49
Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Irhaab, uk. 11-12
Imechapishwa: 02/04/2017
https://firqatunnajia.com/03-kufanya-uasi-kwa-watawala-ni-mfano-wa-ugaidi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)