11 – Tambua – Allaah akurehemu – ya kwamba hakuna kutumia kipimo katika Sunnah, hazipigiwi mfano kwa kitu na wala hazifuatwi kwa matamanio. Badala yake inahusiana na kusadikisha masimulizi yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pasi na kuulizia namna na wala maelezo. Wala mtu asiseme “Kwa nini?” au “Vipi?”.
12 – Falsafa, magomvi, mijadala na ubishi yote ni mambo yaliyozuliwa. Mambo hayo yanatia shaka ndani ya moyo ingawa mwenye kufanya hivo atapatia haki na akazungumza kwa mujibu wa ´Aqiydah.
13 – Tambua – Allaah akurehemu – ya kwamba kuchunguza juu ya Mola ni jambo la kizushi, Bid´ah na upotevu. Hakuzungumzwi juu ya Mola isipokuwa kwa yale aliyojisifia Mwenyewe ndani ya Qur-aan na yale Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyowabainishia Maswahabah zake. Hakika Yeye (´Azza wa Jall) ni Mmoja:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[1]
14 – Mola wetu ni wa Mwanzo, bila kuwa na mwanzo, na ni wa Mwisho, bila kuwa na kikomo. Anayajua ya siri na yaliyofichikana. Amelingana juu ya ´Arshi. Ujuzi Wake uko kila mahali na hakuna mahali unakosekana.
15 – Hakuna mwenye kusema kuhusu sifa za Allaah “Vipi” au “Kwa nini” isipokuwa yule mwenye shaka juu ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).
16 – Qur-aan ni maneno ya Allaah, uteremsho na nuru Yake. Haikuumbwa, kwa sababu Qur-aan inatokamana na Allaah na chenye kutokamana na Allaah hakikuumbwa hakiwi kiumbe. Hivyo ndivyo alivosema Maalik bin Anas, Ahmad bin Hanbal na wanazuoni kabla na baada yao. Kujadiliana juu yake ni kufuru.
[1] 42:11
- Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 70-71
- Imechapishwa: 11/12/2024
11 – Tambua – Allaah akurehemu – ya kwamba hakuna kutumia kipimo katika Sunnah, hazipigiwi mfano kwa kitu na wala hazifuatwi kwa matamanio. Badala yake inahusiana na kusadikisha masimulizi yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pasi na kuulizia namna na wala maelezo. Wala mtu asiseme “Kwa nini?” au “Vipi?”.
12 – Falsafa, magomvi, mijadala na ubishi yote ni mambo yaliyozuliwa. Mambo hayo yanatia shaka ndani ya moyo ingawa mwenye kufanya hivo atapatia haki na akazungumza kwa mujibu wa ´Aqiydah.
13 – Tambua – Allaah akurehemu – ya kwamba kuchunguza juu ya Mola ni jambo la kizushi, Bid´ah na upotevu. Hakuzungumzwi juu ya Mola isipokuwa kwa yale aliyojisifia Mwenyewe ndani ya Qur-aan na yale Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyowabainishia Maswahabah zake. Hakika Yeye (´Azza wa Jall) ni Mmoja:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[1]
14 – Mola wetu ni wa Mwanzo, bila kuwa na mwanzo, na ni wa Mwisho, bila kuwa na kikomo. Anayajua ya siri na yaliyofichikana. Amelingana juu ya ´Arshi. Ujuzi Wake uko kila mahali na hakuna mahali unakosekana.
15 – Hakuna mwenye kusema kuhusu sifa za Allaah “Vipi” au “Kwa nini” isipokuwa yule mwenye shaka juu ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).
16 – Qur-aan ni maneno ya Allaah, uteremsho na nuru Yake. Haikuumbwa, kwa sababu Qur-aan inatokamana na Allaah na chenye kutokamana na Allaah hakikuumbwa hakiwi kiumbe. Hivyo ndivyo alivosema Maalik bin Anas, Ahmad bin Hanbal na wanazuoni kabla na baada yao. Kujadiliana juu yake ni kufuru.
[1] 42:11
Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 70-71
Imechapishwa: 11/12/2024
https://firqatunnajia.com/03-kuamini-na-kusadikisha-bila-ya-kuhoji-maswali/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)