Allaah amemdhamini yule mwenye kuwafuata Wahajiri na Wanusuraji – kwa sharti hii – kwa wema, bi maana kwa ustadi. Sio mtu madai au kujinasibisha tu pasi na ujuzi, ima mtu akafanya hivo kwa ujinga au kwa matamanio. Sio kila mwenye kujinasibisha na Salaf anakuwa Salafiy, mpaka awe anawafuata kwa wema. Hii ni sharti iliyowekwa na Allaah (´Azza wa Jall).
Hii inatakikana kwa wafuasi wausome mfumo wa Salaf, wautambue na washikamane nao barabara. Kujinasibisha nao tu na wakati huohuo mtu akawa hajui mfumo wala ´Aqiydah yao, hili halifidishi kitu. Huyu si katika Salaf na wala sio Salafiy. Hakuwafuata Salaf kwa wema, kama Allaah (´Azza wa Jall) alivyoshurutisha. Nyinyi katika chuo kikuu hichi, katika nchi hii na katika misikiti ya nchi hii kinachofunzwa ni mfumo wa Salaf-us-Swaalih. Lengo ni ili mtu aweze kuwafuata kwa wema. Haihusiani na madai na kujiita tu. Ni wangapi wamedai Salafiyyah na kwamba wanafuata mfumo wa Salaf ilihali uhalisia wa mambo ni kwamba sivyo. Hili ni kutokana ima na kutokujua kwake mfumo wa Salaf au kwa sababu ya kufuata matamanio yake; mtu akawa anajua lakini hata hivyo akawa anafuata matamanio yake badala ya kufuata mfumo wa Salaf.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: as-Salafiyyah haqiyqatuhaa wa simaatuhaa, 17-18
- Imechapishwa: 06/05/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket