107- Jaabir ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Usijifunze elimu kwa ajili ya kujifakharisha kwa wanachuoni, kugombana na wapumbavu wala kwa ajili ya kuingia katika vikao vizuri. Yule mwenye kufanya hivo basi ajihadhari na Moto ajihadhari na Moto.”[1]
Ameipokea Ibn Maajah, Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” na al-Bayhaqiy kupitia kwa Yahyaa bin Ayyuub al-Ghaafiqiy, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa Abuz-Zubayr. Yahyaa huyu ni mwaminifu na al-Bukhaariy na Muslim wote wawili wamemjengea hoja na wala hayazingatiwi maoni ya wale wenye kumdhoofisha.
108- Ibn Maajah amepokea mfano wake kupitia kwa Hudhayfah.[2]
[1] Swahiyh kupitia zengine.
[2] Swahiyh kupitia zengine.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/153)
- Imechapishwa: 03/05/2020
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)