586- Qabuus amesimulia kutoka kwa baba yake aliyesema:

“Baba yangu alinituma kwenda kwa ´Aaishah kumuuliza ni swalah gani ambayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapenda kuidhibiti zaidi. Akajibu: “Alikuwa akiswali [Rak´ah] nne kabla ya Dhuhr; akirefusha kwazo kisimamo na akifanya uzuri Rukuu´ na Sujuud.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah.

[1] Nzuri kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/381)
  • Imechapishwa: 09/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy