24 – Shaddaad bin Aws (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Bwana wa du´aa ya msamaha ni:
اللهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لا إِلهَ إِلاَّ أَنْتَ خَلَقْتَنِي وَأَنَا عَبْدُكَ وَأَنا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ أَبوءُ لَكَ بِنِعْمَتِك عَلَيَّ وأَبوءُ بِذَنْبِي فاغْفِرْ لي فإِنَّه لاَ يغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أَنْتَ
“Ee Allaah! Wewe ni Mola wangu. Hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Wewe. Umeniumba mimi na mimi ni mja wako. Nami niko juu ya ahadi Yako na agano lako kiasi cha uwezo wangu. Najikinga Kwako kutokana na shari ya nilichokifanya. Nakiri Kwako kwa kunineemesha. Nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unisamehe kwani hasamehi madhambi isipokuwa Wewe.”
Mwenye kuisoma pindi inapoingia jioni na akafa usiku huo huo anaingia Peponi. Mwenye kuisoma pindi inapoingia asubuhi na akafa mchana huo huo anaingia Peponi.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy.
MAELEZO
Dhikr hii inaitwa ´bwana wa istighfaar`. Kwa maana ya kwamba du´aa hii ndio istighfaar bora, tukufu na yenye kutangulizwa mbele zaidi. Hilo ni kwa sababu imekusanya kumshuhudia Allaah (Ta´ala) umoja, uola na mja kutambua juu ya Allaah kuabudiwa Kwake pekee na mja kutambua dhambi yake na kumuhitaji Kwake Mola Wake. Mja anatafuta ukaribu kwa Allaah kwa mambo yote haya ikiwemo kumuomba msamaha. Kwa ajili hiyo dhikr hii ikawa ni ´bwana wa istighfaar`.
Mja akisema dhikr hii hali ya kujuta na kujivua kunako dhambi ambapo akafa, basi ni katika watu wa Peponi.
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
”Nakiri Kwako kwa kunineemesha.”
Kunajumuisha kumneemesha kwake katika kumsaidia kumtii. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Nakiri kwa madhambi yangu.”
Anabainisha kukiri Kwake madhambi yake ambayo anahitaji kuomba msamaha kwayo. Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kuhurumia na Mwenye kupokea shukurani. Anasamehe kwa dhambi kubwa na anashukuru kwa jambo dogo.”[2]
[1] al-Bukhaariy (6306).
[2] Majmuu´-ul-Fataawaa (01/212).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 29-30
- Imechapishwa: 05/10/2025

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 29-30
Imechapishwa: 05/10/2025
https://firqatunnajia.com/03-bwana-wa-duaa-ya-msamaha/