5 – ´Umar bin Shabbah amenihadithia, kutoka kwa Ibn ´Aaishah, aliyeeleza kwamba ´Abdullaah bin al-Mubaarak amesema:

Pengine yule mwenye mavazi mawili ya zamani kesho

akiwa kwenye nyumba yenye mazulia yaliyotandazwa na  mito yake imetandikwa

Mito yake inapita kwenye jumba lake la kifalme,

kuangazwa na kuzungukwa na bustani zake

6 – al-Husayn bin ´Abdir-Rahmaan amenihadithia: Muhammad bin Suwayd amenihadithia, aliyesema:

”Watu wa al-Madiynah walikumbwa na ukame. Palikuwepo mtu mwema aliyedumu ndani ya msikiti wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Walipokuwa katika du´aa zao, akaja mtu aliyevaa mavazi mawili yaliyopasuka ambapo akaswali Rak´ah mbili fupi. Kisha akainua mikono yake na kusema: ”Ee Mola wangu! Naapa Kwako kwamba ushushe mvua hivi sasa.” Hakuirudisha mikono yake na hakumalizika kuomba du´aa yake mpaka mbingu zikafunikwa na mawingu na kukaanza kunyesha. Mpaka wakazi wa al-Madiynah wakaanza kupiga kelele kwa khofu ya mafuriko. Wakasema: ”Ee Mola wangu, ikiwa unajua kwamba sasa wametosheka na mvua, basi iondoshe kwao.” Mvua ikakoma. Bwana mmoja akamwandama yule mwombaji mvua mpaka alipojua ni wapi anapoishi. Kisha akamwendea asubuhi mapema na kusema: ”Hakika nimekujilia kwa sababu ya haja fulani.” Akasema: ”Ni ipi?” Akasema: ”Niombee du´aa maalum.” Akasema: ”Allaah ametakasika kutokana na mapungufu! Wewe ni wewe halafu unaniomba nikuombee du´aa maalum? Kwani umesikia nini?” Akasema: ”Kile nilichokiona.” Akasema: ”Umeniona?” Akasema: ”Ndio.” Ndipo bwana yule akasema: ”Nimemtii Allaah katika aliloniamrisha na kunikataza. Nikamuomba ndipo akanipa.”

7 – Naswr bin ´Aliy al-Jahdhwamiy amenihadithia: al-Aswma´iy ametuhadithia, kutoka kwa Abu Mawduud, kutoka kwa Muhammad bin al-Munkadir, ambaye ameeleza:

”Nilikuwa msikitini na ghafla nikamuona mtu karibu na mimbari anamuomba Allaah mvua. Mvua ilikuja kwa sauti kali na radi. Akasema: ”Ee Mola wangu, siyo namna hii.” Kukanyesha na nikamfuata mpaka akaingia katika nyumba ya famili ya Hizm au familia ya ´Umar. Hivyo nikajua ni wapi anapoishi. Nikaja kesho yake nikamletea kitu, akakataa na akasema: ”Sina haja nacho.” Nikasema: ”Hiji pamoja nami.” Akasema: ”Hilo ni jambo ambalo utapata thawabu na nachukia kukunyima hilo. Ama kitu cha kuchukua, basi siwezi.”

8 – Abu Bakr bin Sahl at-Tamiymiy ametuhadithia: Ibn Abiy Maryam ametuhadithia: Naafiy´ bin Yaziyd ametuhadithia, kutoka kwa ´Ayyaash bin ´Abbaas, kutoka kwa ´Iysaa bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Zayd bin Aslam, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Umar, ambaye ameeleza:

”Aliingia msikitini na tahamaki akamkuta Mu´aadh bin Jabal analia karibu na kaburi la Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akamuuliza: “Ni nini , ee Mu´aadh?” Akasema: “Hadiyth niliyoisikia kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Nimesikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: ”Kujionyesha kidogo ni shirki. Hakika Allaah anawapenda wachaji, wanyenyekevu na wema ambao wanapokosekana hawatambuliki na wanapokuwepo hawajulikani. Nyoyo zao ni taa za uongofu na wanapona kutokana na kila hali ya mchafuko yenye giza.”[1]

[1] al-Haakim (¼ na 4/328), ambaye amesema kuwa ni Swahiyh na adh-Dhahabiy akaafikiana naye. Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwaiyf-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (20, 1636 na 1866).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 24-30
  • Imechapishwa: 21/01/2026