2 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitembea katika njia ya Makkah na akapita karibu na mlima unaoitwa Jumdaan ambapo akasema: ”Huu ni [mlima wa] Jumdaan, endeleeni kwani Mufarriduwn wametangulia mbele.” Wakasema: ”Ni nani hao Mufarraduun?” Akasema: ”Ni wale wanaume na wanawake wanaomtaja Allaah kwa wingi.”[1]

MAELEZO

Bi maana wale waliotangulia katika mambo ya kheri, fadhilah na thawabu. Dhikr inakuwa kwa moyo, mdomo na kwa viungo vya mwili.

Dhikr zinazofanywa kwa viungo vya mwili ni zile ´ibaadah zote. Mswaliji ni mwenye kumtaja Allaah (´Azza wa Jall) na mfungaji anamtaja Allaah (´Azza wa Jall).

Dhikr kwa moyo inakuwa kwa kule kumuadhimisha Allaah (´Azza wa Jall), kumuogopa, kumtukuza, kuzingatia ishara na alama Zake na viumbe Wake. Aidha kwa kumkumbuka kwa kukumbuka amri na makatazo Yake. Ina maana ya kwamba akakumbuka maamrisho Yake ambapo akayafanya, na makatazo Yake ambapo akayaepuka.

Dhikr kwa mdomo ni kama kusema “Subhaan Allaah”, “Alhamdulillaah”, “Laa ilaaha illa Allaah”, “Allaahu Akbar” na mfano wake.

[1] Muslim (2676).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 08
  • Imechapishwa: 24/09/2025