02. Uharamu wa kufunga siku moja au mbili kabla ya Ramadhaan

1- Imeharamishwa kufunga siku moja au mbili kabla ya mwezi kwa lengo la kuchukua lililo salama zaidi kwa ajili ya Ramadhaan. Lakini yule ambaye atakuwa na mazowea ya kufunga swawm fulani – na hakufunga kwa lengo la kusimama palipo salama zaidi kwa ajili ya Ramadhaan – hapana neno akafunga. Mfano wa funga hizo ni yule aliyezowea kufunga jumatatu na alkhamisi na siku hizo zikakutana na mwisho wa mwezi, yule anayefunga swawm ya lazima kama swawm ya nadhiri, swawm ya kafara na swawm ya kulipa siku anazodaiwa Ramadhaan iliotangulia. Hayo ni kutokana na yale yaliyothibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mmoja wenu asiitangulizie Ramadhaan kwa kufunga siku moja au mbili. Isipokuwa mtu ambaye alikuwa akifunga swawm. Basi aiendeleze.”[1]

[1] al-Bukhaariy (1914) na Muslim (1082).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtaswaru fiy Ahkaam-is-Swiyaam, uk. 10
  • Imechapishwa: 10/04/2019