Inasikitisha sana kwa Shaykh Bakr kusema:

“Je, makosa haya yatazuia mchakato ili kisichapishwe?”

Hivi kweli mtu mwenye busara huomba kitu kama hicho? Utakasifu ni wa Yule mwenye kuzipindukia nyoyo. Wapendwa wasomaji! Waulizeni hao wanachuoni niliyowataja kama niliwaomba ombi hilo!

Nilipata sapoti yenye nguvu kutoka kwa wanachuoni wengi waheshimiwa. Kila Salafiy wa kweli – katika wanachuoni, wanafunzi na wengi waliodanganyika na Sayyid Qutwub na vitabu vyake – ulimwenguni walifurahia kitabu hichi kilichobarikiwa. Sina shaka kuwa kimekwama kwenye koo za Ahl-ul-Ahwaa´ wengi ambao wanaikataa haki na kushikamana na batili. Watu hawa hakuna la kufanya isipokuwa kuwasikitikia na kuwahurumia. Halafu tukumbuke maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ

“Ukiwatii wengi walioko ulimwenguni watakupoteza na njia ya Allaah.”[1]

Lililokuwa bora kwa Shaykh Bakr alikuwa azuie vitabu ambavyo baadhi yavyo Mtume wa Allaah Muusa anatukanywa, kama ilivyo katika “Taswiyr al-Fanniy”.

Baadhi yavyo vina matusi kwa khaliyfah mwongofu wa tatu ´Uthmaan bin ´Affaan na Maswahabah watukufu walioeshi katika zama zake kama ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf, az-Zubayr bin al-´Awaam na Sa´iyd bin Abiy Waqqaas (Radhiya Allaahu ´anhum).

Baadhi yavyo sifa za Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) zinakanushwa. Humo mna nadharia ya kwamba ulimwengu wote ni Allaah, Ummah mzima ni makafiri na makosa mengine mengi yaliyo kwenye vitabu vya Sayyid Qutwub.

Hili lilikuwa ni bora kwake kwa kuzingatia ya kwamba ni mwenye kuandaa Salaf na mfumo wao mkubwa ambao Allaah amehifadhi haki kwayo na kuitweza batili.

[1] 06:116