02. Nuskha nyingi ya kitabu kimoja    

Wanachuoni waliwaamrisha wanafunzi kulinda vitabu kutokamana na mageuzo na mabadiliko. Kitabu kinaandikwa na kunakiliwa. Nakala ikiwa sahihi basi na kitabu pia kinakuwa sahihi. Ikiwa uandikaji na nakala haiko vizuri basi elimu inaingiliwa. Kwa ajili hiyo wakasema watunzi wengi, ikiwa ni pamoja vilevile na al-Jaahidh katika kitabu “al-Hayawaan”, ya kwamba kuna wanachuoni ambao walikuwa wakinunua nuskha ya vitabu vitatu ya kitabu hicho hicho kimoja. Na kama mapokezi yalikuwa mengi walikuwa wanaweza kuzidisha idadi hiyo kwa ajili ya kupata mapokezi yote yaliyopokelewa na kitabu. Yote haya ilikuwa ni kwa ajili ya kuitilia elimu umuhimu mkubwa na ufunzaji sahihi. Kuna uwezekano nuskha hizo tofauti zikawa zinatofautiana katika maneno na sentesi na kile kilichoandikwa kimakosa katika nuskha moja kimeandikwa sahihi katika nuskha nyingine.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Twaalib-ul-´Ilm wal-Kutub
  • Imechapishwa: 03/05/2020