Swali 2: Kuna wanaosema:
”Imani ni maneno, vitendo na kuamini. Lakini matendo ni sharti la kuikamilisha.”
na:
”Hakuna kufuru isipokuwa kwa kuamini.”
Je, matamshi haya ni kwa mujibu wa Ahl-us-Sunnah?
Jibu: Haya maneno sio ya Ahl-us-Sunnah. Ahl-us-Sunnah wanasema kuwa imani ni maneno ya ulimi, maneno ya moyo, matendo ya viungo vya mwili na matendo ya moyo. Wanao msemo mwingine kwamba imani ni maneno na matendo. Wanao msemo wa tatu kwamba imani maneno, matendo na nia. Hivyo imani lazima iwe na vitu hivi vinne:
1 – Maneno ya ulimi, ambayo ni kule kutamka kwa ulimi.
2 – Matendo ya moyo, ambayo ni kukubali na kusadikisha.
3 – Matendo ya moyo, ambayo ni nia na ikhlaasw.
4 – Matendo ya viungo vya mwili.
Kwa hivyo matendo ni sehemu ya imani na si kwamba matendo ni sharti la kuikamilisha au kwamba ni yenye kulazimiana nayo. Haya ni matamshi ya Murji-ah. Hatutambui kuwa kuna Ahl-us-Sunnah waliosema kuwa matendo ni sharti kuikamilisha imani.
Vilevile wanaosema kwamba hakuna kufuru isipokuwa kwa kuamini. Hayo ni maneno ya Murji-ah. Miongoni mwa maneno yao mengine ni kwamba:
”Matendo na maneno ni ushahidi wa zile I´tiqaad zilizomo moyoni.”
Ni batili. Bali maneno ya kufuru yenyewe kama yenyewe ni kufuru, kitendo cha kufuru chenyewe kama chenyewe ni kufuru, kama ilivyotangulia katika maneno Yake Allaah (Ta´ala):
قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ
“Sema: Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayah Zake na Mtume Wake?” Msitoe udhuru; mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.”[1]
Kwa maana ya kwamba mmeshakufuru kwa maneno yenu.
[1] 09: 65-66
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 06-08
- Imechapishwa: 31/12/2025
Swali 2: Kuna wanaosema:
”Imani ni maneno, vitendo na kuamini. Lakini matendo ni sharti la kuikamilisha.”
na:
”Hakuna kufuru isipokuwa kwa kuamini.”
Je, matamshi haya ni kwa mujibu wa Ahl-us-Sunnah?
Jibu: Haya maneno sio ya Ahl-us-Sunnah. Ahl-us-Sunnah wanasema kuwa imani ni maneno ya ulimi, maneno ya moyo, matendo ya viungo vya mwili na matendo ya moyo. Wanao msemo mwingine kwamba imani ni maneno na matendo. Wanao msemo wa tatu kwamba imani maneno, matendo na nia. Hivyo imani lazima iwe na vitu hivi vinne:
1 – Maneno ya ulimi, ambayo ni kule kutamka kwa ulimi.
2 – Matendo ya moyo, ambayo ni kukubali na kusadikisha.
3 – Matendo ya moyo, ambayo ni nia na ikhlaasw.
4 – Matendo ya viungo vya mwili.
Kwa hivyo matendo ni sehemu ya imani na si kwamba matendo ni sharti la kuikamilisha au kwamba ni yenye kulazimiana nayo. Haya ni matamshi ya Murji-ah. Hatutambui kuwa kuna Ahl-us-Sunnah waliosema kuwa matendo ni sharti kuikamilisha imani.
Vilevile wanaosema kwamba hakuna kufuru isipokuwa kwa kuamini. Hayo ni maneno ya Murji-ah. Miongoni mwa maneno yao mengine ni kwamba:
”Matendo na maneno ni ushahidi wa zile I´tiqaad zilizomo moyoni.”
Ni batili. Bali maneno ya kufuru yenyewe kama yenyewe ni kufuru, kitendo cha kufuru chenyewe kama chenyewe ni kufuru, kama ilivyotangulia katika maneno Yake Allaah (Ta´ala):
قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ
“Sema: Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayah Zake na Mtume Wake?” Msitoe udhuru; mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.”[1]
Kwa maana ya kwamba mmeshakufuru kwa maneno yenu.
[1] 09: 65-66
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 06-08
Imechapishwa: 31/12/2025
https://firqatunnajia.com/02-matendo-ni-katika-imani-si-sharti-la-kuikamilisha/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket