8 – Muhammad bin ´Umar bin Yuusuf ametuhadithia: Israa’iyl ametuhadithia: Simaak ametuhadithia, kutoka kwa Musw´ab bin Sa´d, kutoka kwa baba yake Sa´d bin Abiy Waqqaas, ambaye amesema:
”Kuliteremshwa juu yangu Aayah nne kutoka katika Kitabu cha Allaah (Ta´ala). Mama yangu aliapa kuwa hatokula wala kunywa mpaka niachane na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ndipo Allaah (Ta´ala) akateremsha:
وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖ وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا
“Wakikufanyia juhudi kwamba unishirikishe na yale usiyokuwa na elimu nayo, basi usiwatii. Lakini suhubiana nao kwa wema duniani.”[1]
Ya pili ni kwamba nilikuwa nimechukua upanga niliokuwa naupenda na nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Nipe upanga huu.” Ndipo kukateremshwa:
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ
”Wanakuuliza kuhusu mali ya mateka.”[2]
Ya tatu ni kwamba wakati nilipokuwa mgonjwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akanitembelea, ambapo nikasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Mimi nataka kuigawa mali yangu. Je, niache wasia wa kutoa nusu yake?” Akasema: ”Hapana.” Nikasema: ” Vipi theluthi yake?” Akanyamaza na baada ya hapo ikawa inafaa kuacha wasia wa theluthi.
Ya nne ni kwamba nilikunywa pombe na kundi moja katika Answaar ambapo mtu mmoja akanipiga pua yangu kwa taya ya ngamia. Nikamwendea Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na baada ya hapo ndipo Allaah (Ta´ala) akateremsha maharamisho ya pombe.”
[1] 31:15
[2] 8:1
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 108-109
- Imechapishwa: 16/12/2024
8 – Muhammad bin ´Umar bin Yuusuf ametuhadithia: Israa’iyl ametuhadithia: Simaak ametuhadithia, kutoka kwa Musw´ab bin Sa´d, kutoka kwa baba yake Sa´d bin Abiy Waqqaas, ambaye amesema:
”Kuliteremshwa juu yangu Aayah nne kutoka katika Kitabu cha Allaah (Ta´ala). Mama yangu aliapa kuwa hatokula wala kunywa mpaka niachane na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ndipo Allaah (Ta´ala) akateremsha:
وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖ وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا
“Wakikufanyia juhudi kwamba unishirikishe na yale usiyokuwa na elimu nayo, basi usiwatii. Lakini suhubiana nao kwa wema duniani.”[1]
Ya pili ni kwamba nilikuwa nimechukua upanga niliokuwa naupenda na nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Nipe upanga huu.” Ndipo kukateremshwa:
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ
”Wanakuuliza kuhusu mali ya mateka.”[2]
Ya tatu ni kwamba wakati nilipokuwa mgonjwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akanitembelea, ambapo nikasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Mimi nataka kuigawa mali yangu. Je, niache wasia wa kutoa nusu yake?” Akasema: ”Hapana.” Nikasema: ” Vipi theluthi yake?” Akanyamaza na baada ya hapo ikawa inafaa kuacha wasia wa theluthi.
Ya nne ni kwamba nilikunywa pombe na kundi moja katika Answaar ambapo mtu mmoja akanipiga pua yangu kwa taya ya ngamia. Nikamwendea Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na baada ya hapo ndipo Allaah (Ta´ala) akateremsha maharamisho ya pombe.”
[1] 31:15
[2] 8:1
Mhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 108-109
Imechapishwa: 16/12/2024
https://firqatunnajia.com/02-kuwatendea-wema-wazazi-washirikina-muda-wa-kuwa-hawajakuamrisha-maasi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)