Mlango kuhusu maneno (Ta´ala) Yake:
وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ إِحْسَانًا
”Tumemuusia mtu kuwatendea wema wazazi wake wawili.”[1]
1 – Abul-Waliyd Hishaam bin ´Abdil-Malik ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa al-Waliyd bin al-´Ayzaar: Nimemsikia Abu ´Amr ash-Shaybaaniy akisema: Nimemsikia bwana wa nyumba hii – akaashiria nyumba ya ´Abdullaah – yaani Ibn Mas´uud – akisema:
”Nilimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kitendo kipi kinachopendeza zaidi kwa Allaah (Ta´ala).” Akajibu: “Kuswali ndani ya wakati wake.” Nikasema: “Kisha kipi?” Akasema: “Kuwatendea wema wazazi wawili.” Nikasema: “Kisha kipi?” Akasema: “Kupambana jihaad katika njia ya Allaah.” Lau ningeendelea kuuliza basi angeendelea kunijibu.”
2 – Aadam bin Abiy Iyaas ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia: al-Waliyd ametuhadithia: Nimemsikia Abu ´Amr ash-Shaybaaniy akisema: Bwana wa nyumba hii – akaashiria nyumba ya ´Abdullaah – yaani Ibn Mas´uud – ametukhabarisha:
”Nilimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)… ”
3 – Abu Nu´aym ametuhadithia: al-Mas´uudiy ametuhadithia: Ibn-ul-´Ayzaar amenihadithia, kutoka kwa Abu ´Amr ash-Shaybaaniy, kutoka kwa ´Abdullaah, ambaye amesema:
”Nilimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kitendo kipi kinachopendeza zaidi.” Akajibu: “Kuswali ndani ya wakati wake.” Nikasema: “Kisha kipi, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Kuwatendea wema wazazi wawili.” Nikasema: “Kisha kipi?” Akasema: “Kupambana jihaad katika njia ya Allaah.” Halafu akanyamaza. Laiti ningeendelea kuuliza basi angeendelea kunijibu.”
4 – Qutaybah bin Sa´iyd ametuhadithia: Jariyr ametuhadithia, kutoka kwa al-Hasan bin ´Ubaydillaah, kutoka kwa Abu ´Amr ash-Shaybaaniy, kutoka kwa Ibn Mas´uud, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Matendo bora zaidi – kitendo bora zaidi – ni kuswali ndani ya wakati wake na kuwatendea wema wazazi wawili.”
5 – Qays bin Hafsw amenihadithia: ´Abdul-Waahid ametuhadithia: al-Hasan bin ´Ubaydillaah ametuhadithia, kutoka kwa Abu ´Amr, kutoka kwa ´Abdullaah, ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Kitendo bora zaidi ni kuswali ndani ya wakati na kupambana jihaad katika njia ya Allaah.”
Ameipokea pia ´Ubayd al-Muktib, kutoka kwa Abu ´Amr ash-Shaybaaniy, kutoka kwa mmoja katika Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
6 – Abu Nu´aym ametuhadithia, kutoka kwa Israa’iyl, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa Abul-Ahwasw, kutoka kwa Ibn Mas´uud, ambaye amesema:
”Nilimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni matendo yepi bora zaidi? Akasema: ”Kuswali ndani ya wakati, kuwatendea wema wazazi wawili na kupambana jihaad katika njia ya Allaah.” Laiti ningeendelea kuuliza basi angeendelea kunijibu.”
7 – Abun-Nu´maan na Muusa bin Ismaa´iyl wametuhadithia mfano wa hayo: ´Abdul-´Aziyz – yaani Ibn Muslim – ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa Abul-Ahwasw, kutoka kwa Ibn Mas´uud, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] 46:15
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 104-107
- Imechapishwa: 16/12/2024

Mhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 104-107
Imechapishwa: 16/12/2024
https://firqatunnajia.com/01-watendeeni-wema-wazazi-wenu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)