1- Kufunga ni wajibu kwa kila muislamu ambaye kishabaleghe, yuko na akili, muweza na ni mkazi.
2- Kafiri hafungi na wala si wajibu kwake kulipa pindi ataposilimu.
3- Mdogo ambaye bado hajabaleghe sio wajibu kwake kufunga. Lakini ni vizuri aamrishwe ili ajizoweze.
4- Mwendawazimu si lazima kwake kufunga wala kulishiziwa hata kama atakuwa mzee. Vivyo hivyo punguani wa akili ambaye hawezi kupambanua. Kadhalika mzee anayeropoka ambaye hawezi kupambanua.
5- Kushindwa kufunga kwa sababu yenye kudumu. Kama mfano wa mzee na maradhi yasiyotarajiwa kupona. Watu kama hawa wanatakiwa kutolewa chakula kulisha masikini kwa kila siku moja.
6- Mtu ambaye amepatwa na maradhi ya ghafla anayesubiri kupona. Atakula iwapo swawm itakuwa nzito kwake na atalipa baada ya kupona kwake.
7- Mwanamke mwenye mimba au mnyonyeshaji pale swawm itapokuwa nzito kwao kwa sababu ya ujauzito, kunyonyesha au wakachelea juu ya watoto wao. Katika hali hii wanaweza wakala na wakalipa pale itapokuwa wepesi kwao na khofu ikawaondoka.
8- Mwenye hedhi na nifasi hawatofunga katika kile kipindi cha hedhi na nifasi. Watatakiwa kulipa yale yaliyowapita.
9- Aliyelazimika kufungua kwa sababu ya kumuokoa aliyezama au anayeungua. Atafungua ili amuokoe na baadaye atalipa.
10- Msafiri akitaka atafunga na akitaka ataacha kufunga na baadaye atalipa zile siku alizoacha kufunga. Ni mamoja iwe ni safari iliyojitokeza, kama vile safari ya ´Umrah, au ni safari ya kila siku, kama watu wa magari ya kukodi (teksi na mercedes). Wakitaka watakula midhali hawako katika miji yao.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Nubadh fiys-Swiyaam, uk. 02-03
- Imechapishwa: 14/05/2018

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Nubadh fiys-Swiyaam, uk. 02-03
Imechapishwa: 14/05/2018
https://firqatunnajia.com/02-kugawanyika-kwa-watu-katika-swawm/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)