8 – Abu Kurayb ametukhabarisha: Rishdayn bin Sa´d ametukhabarisha, kutoka kwa ´Aqiyl, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin al-Haarith bin Hishaam, kutoka kwa baba yake, ambaye amesema kuwa Mtume wa Allaah (Swallaa Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ee Mtume wa Allaah, nieleze juu ya jambo ambalo nitalishikilia?” Akasema: ”Udhabiti huu.” Akaashiria kwenye ulimi wake.”[1]

9 – Husayn bin Hasan ametukhabarisha: Ibn-ul-Mubaarak ametukhabarisha: Ibn Lahiy´ah ametuhadithia: Khaalid bin Abiy ´Imraan amenikhabarisha:

“Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliushika ulimi wake kwa muda mrefu kisha akautoa na akasema: “Nakhofia kwenu hii.” Alisema hivo mara mbili. Kisha akasema: “Allaah amrehemu mja anayesema kheri na akalipwa kwalo au akanyamaza juu ya maovu na hivyo akasalimika.”[2]

10 – Abu Muusa ametukhabarisha: ´Iysaa bin Shu´ayb Abul-Fadhwl adh-Dhwariyr ametukhabarisha: ar-Rabiy´ bin Sulaymaan an-Numayriy ametukhabarisha, kutoka kwa ´Amr, mtumwa wa Anas bin Maalik, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuuchunga ulimi wake basi Allaah atasitiri aibu yake. Mwenye kuzuia ghadhabu zake, Allaah humzuilia adhabu Yake.”[3]

11 – Abu Bakr ametukhabarisha: Wakiy´ ametukhabarisha, kutoka kwa al-A´mash… (ح) Ibn Numayr pia ametukhabarisha: Wakiy´ ametukhabarisha, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Abu Sufyaan, kutoka kwa Jaabir, aliyesema:

“Mtu mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na akasema: “Ni waislamu gani walio bora zaidi?” Akasema: “Yule ambaye waislamu wamesalimika kwa ulimi na mkono wake.”[4]

12 – Abu Bakr bin Abiy Shaybah ametukhabarisha: Ghundar ametukhabarisha, kutoka kwa Shu´bah, kutoka kwa ´Amr bin Murrah, kutoka kwa ´Abdullaah bin al-Haarith, kutoka kwa Abu Kathiyr, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr, ambaye ameeleza:

”Mtu mmoja alisimama na kusema: “Ee Mtume wa Allaah, ni Uislamu upi ulio bora zaidi?” Akasema: “Waislamu wasalimike kutokana na ulimi na mkono wako.”[5]

13 – Ibn Numayr ametukhabarisha: Ya´laa ametukhabarisha, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Abu Sa´iyd, ambaye amesimulia kuwa:

“Bwana mmoja alikuja kwa ´Abdullaah bin ‘Amr na akasema: “Tunataka kukuuliza juu ya jambo ambalo umesikia kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Akasema: “Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Muislamu ni yule ambaye waislamu wamesalimika kwa ulimi na mkono wake.”[6]

14 – Abu Kurayb ametukhabarisha: Abu Khaalid al-Ahmar ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn ´Ajlaan, kutoka kwa Abu Haazim, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kuhifadhi kile kilocho baina ya taya zake na miguu yake ataingia Peponi.”[7]

[1] at-Twabaraaniy (3349). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (1391).

[2] Ibn-ul-Mubaarak katika “az-Zuhd”, uk. 128. Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ul-Jaamiy´” (98).

[3] Abu Ya´laa (4338). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “as-Swahiyhah” (2360).

[4] al-Bukhaariy (6484) na Muslim (41).

[5] Ahmad (6451). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (2604).

[6] al-Bukhaariy (10) na Muslim (40).

[7] al-Haakim (4/398). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (6593).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 7-8
  • Imechapishwa: 24/06/2025