1007- Thawbaan (Radhiya Allaahu ´anh), mtumwa wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyeachwa huru, ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kufunga siku sita baada ya Fitwr anazingatiwa amefunga mwaka mzima:

مَن جَاء بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا

“Yule anayekuja kwa jema moja, basi analipwa kumi mfano wake.”[1][2]

Ameipokea Ibn Maajah na an-Nasaa´iy ambaye yeye tamko lake ni kama ifuatavyo:

“Allaah amefanya jema moja mtu analipwa kumi mfano wake. Mwezi mmoja mtu analipwa miezi kumi. Kufunga siku sita baada ya Fitwr anazingatiwa amefunga mwaka mzima.”[3]

Vilevile ameipokea Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake. Tamko ni lake na pia ni moja katika mapokezi ya an-Nasaa´iy:

“Kufunga mwezi wa Ramadhaan mtu analipwa miezi kumi na kufunga siku sita za Shawwaal mtu analipwa miezi miwili. Hiyo inakuwa kufunga mwaka mzima.”[4]

Ibn Hibbaan ameipokea katika “as-Swahiyh” yake na tamko lake linasema:

“Yule mwenye kufunga Ramadhaan na [siku] sita za Shawwaal basi amefunga mwaka mzima.”[5]

1008- Ameipokea Ahmad, al-Bazzaar na at-Twabaraaniy kupitia kwa Jaabir bin ´Abdillaah[6].

[1] 6:160

[2] Swahiyh.

[3] Swahiyh.

[4] Swahiyh.

[5] Swahiyh.

[6] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/589)
  • Imechapishwa: 09/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy