02. Hadiyth ”Mwelezeni kuwa Allaah anampenda… ”

Hadiyth ya kwanza

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ

“Sema: ”Allaah ni Mmoja pekee.”[1]

1 – Shaykh Abul-Fadhwl Ahmad bin Hibatillaah bin Ahmad bin Muhammad ad-Dimashqiy ametukhabarisha, kutoka kwa Abul-Mudhwaffar as-Sam´aaniy: ´Abdullaah al-Furaawiy ametuhadithia: ´Uthmaan bin Muhammad Abu ´Amr al-Muhammiy ametuhadithia: Abu Nu´aym al-Ashariy ametuhadithia: Abu ´Awaanah al-Haafidhw ametuhadithia: Abu ´Ubaydillaah, mpwa wa Ibn Wahb, ametuhadithia: Ami yangu ´Abdullaah bin Wahb ametuhadithia: ´Amr bin al-Haarith ametuhadithia, kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Hilaal: Abur-Rijaal amemuhadithia kutoka kwa mama yake ´Amrah, kutoka kwa ´Aaishah ambaye amesema:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimteua bwana mmoja kuwa kiongozi wa msafara wa kijeshi. Alikuwa akiwaswalisha marafiki zake ndani ya swalah na akimalizia kwa:

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ

“Sema: ”Allaah ni Mmoja pekee.”

Waliporudi, wakamweleza hilo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye akasema: ”Muulizeni kwa nini anafanya hivo.” Wakamuuliza ambapo akajibu: ”Kwa sababu ni sifa ya Mwingi wa rehema (´Azza wa Jall). Ndio maana mimi napenda kuisoma. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Mwelezeni kuwa Allaah anampenda.”[2]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Ibn Wahb.

Hakuna mtu yeyote katika wale wanaoswali kuelekea Qiblah ambaye ameipinga sifa hii.

[1] 112:1

[2] al-Bukhaariy (7375) na Muslim (813).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy (afk. 748)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 31-33
  • Imechapishwa: 28/05/2024