´Aqiydah sahihi ni ile aliyokuja nayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akalingania kwayo. Amebainisha (´alayhis-Swalaatu was-Salaam):
“Ummah utafarikiana baada yangu katika mapote sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu. Kukaulizwa: “Ni wepi hao, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni wale wataofuata mfano wa yale ninayofuata mimi hii leo na Maswahabah zangu.”[1]
Yule ambaye ´Aqiydah yake itakuwa ni yenye kuafikiana na yale aliyokuwa akifuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake, basi huyo ndiye ambaye ataokoka na adhabu ya Allaah na ataingia Peponi. Ndio maana pote lililoshikamana na kuwa imara juu ya ´Aqiydah hii likaitwa “Kundi lililookoka” (Firqat-un-Naajiyah). Imeitwa jina hili kwa sababu limeokoka na adhabu ya Allaah miongoni mwa mapote sabini na tatu. Kuhusu mapote mengine yote yataingia Motoni.
Kwa hivyo kundi lililookoka ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hali itaendelea kuwa hivyo daima. Kuanzia kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake mpaka mwisho wa Ummah huu wa Muhammad pale ambapo Qiyaamah kitasimama. Imethibiti katika Hadiyth isemayo:
“Hakutoacha kuwepo kipote katika Ummah wangu kuwa juu ya haki hali ya kuwa ni chenye kushinda. Hakitodhurika na wale wenye na wenye kwenda kinyume nao mpaka kifike Qiyaamah na wao wamo katika hali hiyo.”[2]
[1] Abu Daawuud (4597), Ahmad (04/102) na ad-Daarimiy (2518).
[2] Muslim (1920), at-Tirimidhiy (2229), Abu Daawuud (4252), Ibn Maajah (10) na Ahmad (05/279).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Mujmal ´Aqiydat-is-Salaf as-Swaalih, uk. 03
- Imechapishwa: 24/05/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)