01- Ni lazima kwa mgonjwa kuridhia makadirio ya Allaah, asubirie yale aliyomkadiria na amdhanie vyema. Kwani hayo ni kheri kwake. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ajabu ilioje juu ya jambo la muumini. Kwani hakika mambo yake yote kwake ni kheri – na hayo hayawi kwa mwingine isipokuwa kwa muumini tu – anapofikwa na furaha basi anashukuru na inakuwa ni kheri kwake na anapofikwa na dhara anakuwa na subira na inakuwa ni kheri kwake.”

“Asife mmoja wenu isipokuwa katika hali ya kumdhania Allaah (Ta´ala) vizuri.”

Ameipokea Muslim, al-Bayhaqiy na Ahmad.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 03
  • Imechapishwa: 25/12/2018