Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah ambaye amefanya katika kila zama kuwepo wanazuoni katika kipindi na kusita ujio wa Mitume. Wanawalingania waliopotea katika uongofu na wanasubiri juu ya maudhi yao. Wanahuisha kwa Kitabu cha Allaah wale wafu, na wanawafanya kuweza kuona kwa nuru ya Allaah wale vipofu. Ni wangapi waliouliwa na Ibliys wamewahuisha! Ni wapotofu wangapi waliodanga ambao wamewaongoza! Ni athari nzuri iliyoje walionao kwa watu na ni ubaya uliyoje athari ya watu dhidi yao! Wanakilinda Kitabu cha Allaah upotoshaji wa waliochupa mipaka, madai ya watu wa batili na upindishaji wa maana wa wajinga; watu ambao wamechochewa kwa bendera za Bid´ah na kufungua njia za fitina. Wametofautiana juu ya Kitabu, wanaenda kinyume na Kitabu na wamekusanyika juu ya kufarikiana na Kitabu. Wanasema juu ya Allaah na juu ya Kitabu cha Allaah pasi na elimu. Wanazungumza maneno yasiyokuwa wazi na wanawahaa wajinga katika watu katika wanayowababaisha. Tunamuomba Allaah ulinzi kutokana na fitina zinazopotosha.

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 55-57
  • Imechapishwa: 02/04/2024