01. Utangulizi wa ”Ithaaf Ahl-il-Iymaan”

Himdi zote njema ni stahiki ya ambaye Ameweka kwa waja Wake Shari´ah ya kufunga mwezi wa Ramadhaan na akaifanya kuwa ni moja ya nguzo za Uislamu. Swalah na salamu zimshukie Nabii wetu Muhammad – mbora kuliko wote aliyeswali na aliyefunga – na juu ya watu wa nyumba yake na Maswahabah wake wema watukufu.

Ama baada ya hayo;

Haya ni mafunzo yanayohusisha kukumbushana fadhilah za mwezi huu uliobarikiwa na kuhimiza kufanya juhudi na bidii ndani yake, kuitumia vyema michana na nyusiku zake, pamoja na kuashiria baadhi ya hukumu za ki-Fiqh zinazohusiana na swawm na kusimama usiku. Nimekusudia kuyaandika kama ukumbusho kwangu binafsi na kwa ndugu zangu hali ya kumuomba Allaah anufaishe kwa yaliyomo aliyeandika, aliyeyasoma na aliyeyasikia miongoni mwa waislamu na anisamehe yaliyojitokeza ndani yake ya makosa au upungufu.

Ee Allaah! Msifu na msalimu Nabii wetu Muhammad, jamaa zake na Maswahabah wake.

Mtunzi

Tarehe 09 Swafar 1408

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 9
  • Imechapishwa: 24/01/2026