Himdi zote anastahiki Allaah ambaye ametuongoza katika Uislamu, kutuneemesha nao na kutufanya kuwa katika ummah bora. Tunamuomba mafanikio katika yale anayoyapenda na kuyaridhia pamoja na kutuhifadhi kutokamana na yale anayoyabughudhi na kuyachukia.
1 – Tambua ya kuwa Uislamu ndio Sunnah na Sunnah ndio Uislamu na kimojawapo hakisimami isipokuwa kwa kingine.
2 – Ni katika Sunnah kulazimiana na Mkusanyiko. Yule ambaye hataki kuwa katika Mkusanyiko na akatengana nayo, basi ameivua kamba ya Uislamu katika shingoni mwake na atakuwa ni mpotevu mwenye kupoteza.
3 – Msingi ambao Mkusanyiko umejengwa juu yake ni Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Nao ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Yule asiyechukua kutoka kwao basi amepotea na kuzusha. Kila Bid´ah ni upotevu na upotevu na watu wake ni Motoni.
4 – ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Hakuna udhuru kwa yeyote aliyeingia ndani ya upotevu huku akidhania kuwa ni uongofu, na wala uongofu aliouacha huku akidhania kuwa ni upotevu. Mambo yamebainishwa, hoja zimethibiti na udhuru umekatika.”[1]
Hili ni kwa sababu Sunnah na Mkusanyiko vimekamilisha mambo ya dini yote. Hivi sasa yamebainishwa kwa watu. Hivyo basi ni wajibu kwa watu kufuata tu.
5 – Tambua – Allaah akurehemu – ya kwamba dini ni yenye kutoka kwa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Haikuachwa kwenye akili na maoni ya wanaume. Elimu yake ni kutoka kwa Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivyo usifuate kitu katika matamanio yako ukaja kutoka katika dini na kutoka katika Uislamu. Hakika huna hoja yoyote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewabainishia ummah wake Sunnah na akawawekea nayo wazi Maswahabah zake – nao ndio Mkusanyiko na Kundi kubwa. Kundi kubwa ni haki na watu wake. Kwa hivyo yule mwenye kwenda kinyume na Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika jambo la dini, basi amekufuru.
[1] al-Ibaanah al-Kubraa (162) ya Ibn Battwah al-´Ukbariy.
- Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 67-68
- Imechapishwa: 11/12/2024

Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 67-68
Imechapishwa: 11/12/2024
https://firqatunnajia.com/01-uislamu-ndio-sunnah-sunnah-ndio-uislamu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)