01. Namna kilivyokuja “al-Hamawiyyah”

Mwaka wa 698 Shaykh Ahmad bin ´Abdil-Haliym bin ´Abdis-Salaam bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) aliulizwa swali ambalo lilimletea matatizo na mtihani. Ni jibu tukufu lenye faida nyingi sana.

MAELEZO

Moja katika vitabu vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) vyenye manufaa ni hiki kinachoitwa ”al-Fatwaa al-Hamawiyyah al-Kubraa”. Kitabu kimeitwa hivo kwa sababu muulizaji anatokea Hamaa, Shaam. Ni kama mfano wa ”al-Waasitwiyyah” kwa sababu muulizaji anatokea Waasitw, ´Iraaq.

Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) alikuwa na uwezo wa kuandika haraka. Ameeleza mwenyewe namna alivyoandika al-Waasitwiyyah”katika kikao kati ya Dhuhr na ´Aswr. Akijibu swali akaandika kitabu kizima, ndani ya kikao kimoja. Alikuwa na elimu sana. Alikuwa anaweza kuzitoa elimu na kuziandika kwa haraka. Kitabu hiki kinaitwa ”al-Hamawiyyah” kwa sababu muulizaji anatokea Hamaa. Bwana huyu anauliza kitu gani? Anamuuliza kuhusu Aayah za majina na sifa za Allaah zilizotajwa ndani ya Qur-aan na Sunnah, kwa sababu ni maudhui ambayo watu wanaifuatilia sana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 24
  • Imechapishwa: 23/07/2024