Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni wale ambao Allaah amewaongoza katika yale ambayo watu wametofautiana kwayo – kwani Allaah anamwongoza amtakaye katika njia ilionyooka. Sote tunatambua kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametumilizwa kwa haki na dini ya kweli. Uongofu usiokuwa na upotevu ndani yake. Dini ya haki isiokuwa na kukosea ndani yake. Katika zama zake watu walibaki juu ya mfumo huu uliosalimika na ulionyooka. Hali iliendelea kuwa hivo katika zama za makhaliyfah wake waongofu. Lakini baada ya hapo Ummah ukafarikiana mfarakano mkubwa kiasi cha kwamba yakafika mapote sabini na tatu ambapo yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu. Nao ni wale ambao watafuata yale aliokuwa akifuata Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake.
Tunasema kwamba kundi hilo lililookoka ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Wasifu huu hauhitaji maelezo katika kubainisha kwamba wao ndio wako juu ya haki. Kwa sababu wao ndio Ahl-us-Sunnah (watu wa Sunnah) ambao wameshikamana nazo na Ahl-ul-Jamaa´ah (watu waliokusanyika) ambao wamekusanyika juu yake.
Hutopata pote lolote – mbali na wao – isipokuwa utawaona kuwa wako mbali na Sunnah kwa kiwango cha yale waliyoyazusha katika dini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Wala hutopata pote – mbali na wao – isipokuwa utaona kuwa ni wenye kufarikiana katika mapote mbalimbali katika yale wanayoyafuata. Allaah (Ta´ala) amesema kumwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا لَّسْتَ مِنْهُمْ فِي شَيْءٍ ۚ إِنَّمَا أَمْرُهُمْ إِلَى اللَّـهِ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ
“Hakika wale waliofarakisha dini yao na wakawa makundimakundi, huna lolote kuhusiana na wao. Hakika amri yao iko kwa Allaah; halafu atawajulisha kwa yale waliyokuwa wakifanya.”[1]
Kwa hiyo hatuna haja ya kurefusha kuelezea Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Kwa sababu jina hili linatakasa maana kamilifu na kwamba wao ni wenye kushikamana barabara na Sunnah na ni wenye kukusanyika juu yake. Sisi tutafupisha maneno katika nukta zifuatazo:
[1] 06:159
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 07-08
- Imechapishwa: 18/06/2019

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 07-08
Imechapishwa: 18/06/2019
https://firqatunnajia.com/01-makusudio-ya-ahl-us-sunnah-wal-jamaaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)