Hakika watu wengi wamekuwa wajinga juu ya Sunnah nyingi kisha wakaziacha, ambapo wakaanza kuwashutumu wale wanaozifuata na kujaribu kuzihuisha na wakiwatuhumu kwa upotevu wa mbali. Miongoni mwa Sunnah hizo ni kuswali huku mtu amevaa viatu. Hakika imepokelewa kwa mapokezi mengi ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali akiwa amevaa viatu vyake. Isitoshe Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anasema:
لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّـهَ كَثِيرًا
“Hakika mna kigezo kizuri kwa Mtume wa Allaah kwa mwenye kumtaraji Allaah na siku ya Mwisho na akamtaja Allaah kwa wingi.”[1]
Na pia imethibitika kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamrisha kuswali ndani ya viatu. Sambamba na hilo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anasema:
وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ
”Kile alichokupeni Mtume basi kichukueni na kile alichokukatazeni basi kiacheni. Mcheni Allaah! Hakika Allaah ni mkali wa kuadhibu.”[2]
وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا
“Haiwi kwa muumini mwanamme na wala kwa muumini mwanamke pindi Allaah anapohukumu na Mtume Wake jambo lolote iwe wana khiyari katika jambo lao – na yule anayemuasi Allaah na Mtume Wake, basi kwa hakika amepotoka upotofu wa wazi.”[3]
فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
“Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitina au ikawasibu adhabu iumizayo.”[4]
Kwa sababu hiyo nimeona ni vyema kukusanya baadhi ya Hadiyth nilizokutana nazo zinazothibitisha uwekwaji Shari´ah wa kuswali huku mtu amevaa viatu. Allaah ndiye mwenye kuongoza katika haki na Kwake ndiko marejeo na mwisho wa safari yetu.
[1] 33:21
[2] 59:7
[3] 33:36
[4] 24:63
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 5-6
- Imechapishwa: 27/05/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket