Allaah wepesisha, na saidia kwa rehema Zako.
Himdi zote njema anastahiki Allaah. Tunamuhimidi Yeye, kumuomba msaada na msamaha. Tunajilinda kwa Allaah kutokana na shari ya nafsi zetu na uovu wa matendo yetu. Yule aliyeongozwa na Allaah, basi hakuna wa kumpotosha, na yule aliyepotoshwa na Allaah, basi hakuna wa kumwongoza. Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yu peke yake pasi na mshirika, na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake. Ee msifu na msalimie yeye, jamaa zake na Maswahabah zake.
Ama baada ya hayo:
Baadhi ya ndugu waliniomba niwaandikie utangulizi ambao utajumuisha kanuni zilizoenea ambazo zitasaidia kuifahamu Qur-aan na kujua tafsiri yake na maana zake, kupambanua kati ya haki na aina za batili na kuzindua ile dalili ya kukata baina ya maoni mbalimbali. Kwani vitabu vilivyotungwa katika tafsiri za Qur-aan vimesheheni kila kitu, haki ya wazi na batili ya wazi. Elimu ima iwe riwaya iliyonukuliwa kutoka kwaa Aliyekingwa na kukosea (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au maoni inayosapotiwa na dalili inayotambulika. Mbali na haya ima iwe yamefanyiwa ghushi yenye kukataliwa au kilichokatika kwa namna ya kwamba hakitambuliki juu ya kusihi kwake wala thamani yake.
Haja ya ummah ni kubwa mno kuifahamu Qur-aan ambayo ndio kamba ya Allaah madhubuti, ukumbusho wenye hekima na njia iliyonyooka, ambayo kwayo matamanio hayaipotezi na ndimi haziichanganyi, haitopotoshwi kwa kule kuirudiarudia sana, maajabu yake hayakomi na wala wanazuoni hawatosheki nayo. Yule anayezungumza kwayo anasema kweli. Yule anaifanyia kazi na analipwa thawabu. Yule mwenye kuhukumu nayo anafanya uadulifu. Yule mwenye kulingania kwayo anaongozwa katika njia iliyonyooka. Yule dhalimu mwenye kuiacha basi Allaah anamvunja na ambaye atatafuta uwongo kwa isiyokuwa yenyewe basi Allaah atampotosha. Amesema (Ta´ala):
فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَىٰ وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَىٰ وَقَدْ كُنتُ بَصِيرًا قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَىٰ وَقَدْ كُنتُ بَصِيرًا قَالَ كَذَٰلِكَ أَتَتْكَ آيَاتُنَا فَنَسِيتَهَا ۖ وَكَذَٰلِكَ الْيَوْمَ تُنسَىٰ
”Utakapokufikieni kutoka Kwangu uongofu, basi atakayefuata uongofu Wangu hatopotea na wala hatopata mashaka. Atakayepuuza ukumbusho Wangu, basi hakika atapata maisha ya dhiki na tutamfufua siku ya Qiyaamah hali akiwa kipofu. Atasema: “Mola wangu! Mbona Umenifufua kipofu na hali nilikuwa nikiona?” Atasema: “Hivyo ndivyo zilikufikia Aayah Zetu ukazisahau na kadhaalika leo umesahauliwa.”[1]
Amesema (Ta´ala) tena:
يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ كَثِيرًا مِّمَّا كُنتُمْ تُخْفُونَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ قَدْ جَاءكُم مِّنَ اللّهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ يَهْدِي بِهِ اللّهُ مَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَهُ سُبُلَ السَّلاَمِ وَيُخْرِجُهُم مِّنِ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِهِ وَيَهْدِيهِمْ إِلَى صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ
“Enyi watu wa Kitabu! Hakika amekujieni Mtume wetu ambaye anakubainishieni mengi katika yale mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu na anasamehe mengi. Hakika imekujieni kutoka kwa Allaah nuru na Kitabu kinachobainisha; Allaah kwacho anamwongoza yule atakayefuata radhi Zake katika njia za salama na anawatoa katika viza kuingia katika nuru kwa idhini Yake na anawaongoza katika njia iliyonyooka.”[2]
كِتَابٌ أَنْزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَى صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ اللَّهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَوَيْلٌ لِلْكَافِرِينَ مِنْ عَذَابٍ شَدِيدٍ
”Kitabu Tumekiteremsha kwako ili uwatoe watu katika viza kuwaingiza katika nuru kwa idhini ya Mola wao, waelekee katika njia ya Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika, Mwenye kustahiki kuhimidiwa. Allaah ambaye ni Vyake pekee vyote viliyomo katika mbingu na katika ardhi na ole kwa makafiri kutokana na adhabu kali.”[3]
وَلَـٰكِن جَعَلْنَاهُ نُورًا نَّهْدِي بِهِ مَن نَّشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا ۚ وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ صِرَاطِ اللَّـهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ أَلَا إِلَى اللَّـهِ تَصِيرُ الْأُمُورُ
”… lakini tumeijaalia kuwa ni nuru, tunamwongoza kwayo Tumtakaye kati ya waja Wetu. Na hakika wewe bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka – Njia ya Allaah ambaye ni Vyake pekee vyote vilivyomo mbinguni na vyote vilivyomo ardhini. Zindukeni! [Kuwa ni] kwa Allaah pekee yanaishia mambo yote.”[4]
Nimeandika utangulizi huu kwa ufupi kulingana na wepesishaji wa Allaah (Ta´ala). Allaah ndiye mwenye kuongoza katika njia iliyonyooka.
[1] 20:123-126
[2] 5:15-16
[3] 14:1-2
[4] 42:52-53
- Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 15-17
- Imechapishwa: 18/03/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)